Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #zanzibarairportauthority

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Sekta ya Usafiri wa Anga Zanzibar yarekodi mapato ya Sh Bilioni 50 ndani ya miaka Mitatu. Sekta ya usafiri wa anga visiwani Zanzibar imeonyesha ukuaji mkubwa, huku mapato ya viwanja vya ndege yakifikia Shilingi bilioni 50 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikilinganishwa na Sh bilioni 18 Kwa mwaka 2022. Ukuaji huu umetokana na ongezeko la idadi ya abiria na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya usafiri wa anga. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), idadi ya abiria imeongezeka kwa asilimia 23 kutoka abiria milioni 1.9 mwaka 2023 hadi milioni 2.4 mwaka 2024. Maofisa wa mamlaka hiyo wanatarajia idadi hiyo kufikia zaidi ya abiria milioni 2.7 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025. Akizungumza siku ya Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa ZAA, Bw. Seif Abdallah Juma, alisema kuwa mafanikio hayo yametokana na uboreshaji wa huduma katika viwanja vya ndege, ufanisi wa uendeshaji, pamoja na kurejea kwa mashirika ya ndege ya kimataifa kama Air France. Kwa sasa, zaidi ya mashirika 78 ya ndege yanafanya safari kuelekea Zanzibar, na mamlaka inatarajia idadi hiyo kuongezeka zaidi kufikia mwezi Juni na Julai. Chanzo:The Citizen @zaazanzibar #airport #airportauthority #airportrevenue #abeidamanikarumeinternationalairport #zanzibarairportauthority #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKOrqsoM8Vx/?igsh=enR0Nzc4c3BtNTRs *Sekta ya Usafiri wa Anga Zanzibar y...

Aviation Tanzania on Instagram: "Air France yarejesha safari za moja kwa moja Kati ya Zanzibar na Ufaransa. Shirika la Ndege la Air France limeanza tena safari za moja kwa moja kati ya Ufaransa na Zanzibar, kufuatia kuwasili kwa ndege yake aina ya Boeing 787-8 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA). Ndege hiyo iliwasili siku ya jumatatu Mei 26, 2025 majira ya saa 2:57 usiku ikiwa na jumla ya abiria 125. Hii ni safari ya kwanza ya moja kwa moja kufanyika tangu mwezi Machi 2025, wakati shirika hilo lilipositisha kwa muda huduma hizo kutokana na msimu mdogo wa abiria (low season). Kwa mujibu wa ratiba mpya, Air France itakuwa ikifanya safari zake za moja kwa moja mara tatu kwa wiki yaani siku za Jumatano, Alhamisi na Jumamosi huku ikifungua fursa zaidi kwa watalii kutoka Ufaransa na mataifa jirani kutembelea visiwa vya Zanzibar. @zaazanzibar #routeexpansion #airline #airfrance #abeidamanikarumeinternationalairport #zanzibarairportauthority #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKKhjs7MIdP/?igsh=MTR3YjhhMmU0eGw0ZA== *Air France yarejesha safari za ...