Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 29, 2025 at 07:42 AM
https://www.instagram.com/p/DKOrqsoM8Vx/?igsh=enR0Nzc4c3BtNTRs *Sekta ya Usafiri wa Anga Zanzibar yarekodi mapato ya Sh Bilioni 50 ndani ya miaka Mitatu.* Sekta ya usafiri wa anga visiwani Zanzibar imeonyesha ukuaji mkubwa, huku mapato ya viwanja vya ndege yakifikia Shilingi bilioni 50 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikilinganishwa na Sh bilioni 18 Kwa mwaka 2022. Ukuaji huu umetokana na ongezeko la idadi ya abiria na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya usafiri wa anga. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), idadi ya abiria imeongezeka kwa asilimia 23 kutoka abiria milioni 1.9 mwaka 2023 hadi milioni 2.4 mwaka 2024. Maofisa wa mamlaka hiyo wanatarajia idadi hiyo kufikia zaidi ya abiria milioni 2.7 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025. Akizungumza siku ya Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa ZAA, Bw. Seif Abdallah Juma, alisema kuwa mafanikio hayo yametokana na uboreshaji wa huduma katika viwanja vya ndege, ufanisi wa uendeshaji, pamoja na kurejea kwa mashirika ya ndege ya kimataifa kama Air France. Kwa sasa, zaidi ya mashirika 78 ya ndege yanafanya safari kuelekea Zanzibar, na mamlaka inatarajia idadi hiyo kuongezeka zaidi kufikia mwezi Juni na Julai. Chanzo:The Citizen @zaazanzibar #airport #airportauthority #airportrevenue #abeidamanikarumeinternationalairport #zanzibarairportauthority #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments