WATANI WA JADI
WATANI WA JADI
June 9, 2025 at 07:00 PM
🚨 *ZA NDANI KABISA MACHAWA WATIA DOA SAJILI YA MZIZE:* Klabu ya **Zamalek SC** imeonyesha nia ya dhati ya kukamilisha usajili wa *Clement Mzize* kutoka klabu ya *Yanga SC*, hata hivyo, mchakato wa uhamisho huo *umesitishwa kwa muda*, tunaweza kuthibitisha. Kumekuwepo na kuongezeka kwa idadi ya mawakala wanaojitokeza ghafla kwenye mchakato huo, akiwemo *mwanamke aitwaye Jasmine*, ambaye anatajwa kudai malipo makubwa kutoka kwa klabu ya Zamalek, jambo ambalo limeleta sintofahamu. *Mwakala mmoja mashuhuri kutoka Morocco*, ambaye ana mamlaka rasmi kutoka kwa mchezaji husika pamoja na klabu yake kushughulikia moja kwa moja mazungumzo ya uhamisho na Zamalek, *ameonyesha kutoridhishwa na namna suala hili linavyoendeshwa kwa sasa – hasa kutokana na kuingiliwa na watu mbalimbali kutoka upande wa mchezaji – hali iliyomsukuma* kushauri klabu ya Zamalek kusimamisha mchakato huo kwa sasa. Kwa sasa, *hakuna hatua yoyote inayoendelea kuhusu uhamisho wa Clement Mzize*. \#usajili bongo ni pasua kichwa hasa watani
Image from WATANI WA JADI: 🚨 *ZA NDANI KABISA MACHAWA WATIA DOA SAJILI YA MZIZE:*  Klabu ya **Za...

Comments