Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #airportauthority
Posts
🚨 #BREAKING: Indian govt directs Airports Authori...
🚨 #BREAKING: Indian govt directs Airports Authority-run airports to review emergency preparedness p...
Aviation Tanzania on Instagram: "Sekta ya Usafiri wa Anga Zanzibar yarekodi mapato ya Sh Bilioni 50 ndani ya miaka Mitatu. Sekta ya usafiri wa anga visiwani Zanzibar imeonyesha ukuaji mkubwa, huku mapato ya viwanja vya ndege yakifikia Shilingi bilioni 50 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikilinganishwa na Sh bilioni 18 Kwa mwaka 2022. Ukuaji huu umetokana na ongezeko la idadi ya abiria na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya usafiri wa anga. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), idadi ya abiria imeongezeka kwa asilimia 23 kutoka abiria milioni 1.9 mwaka 2023 hadi milioni 2.4 mwaka 2024. Maofisa wa mamlaka hiyo wanatarajia idadi hiyo kufikia zaidi ya abiria milioni 2.7 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025. Akizungumza siku ya Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa ZAA, Bw. Seif Abdallah Juma, alisema kuwa mafanikio hayo yametokana na uboreshaji wa huduma katika viwanja vya ndege, ufanisi wa uendeshaji, pamoja na kurejea kwa mashirika ya ndege ya kimataifa kama Air France. Kwa sasa, zaidi ya mashirika 78 ya ndege yanafanya safari kuelekea Zanzibar, na mamlaka inatarajia idadi hiyo kuongezeka zaidi kufikia mwezi Juni na Julai. Chanzo:The Citizen @zaazanzibar #airport #airportauthority #airportrevenue #abeidamanikarumeinternationalairport #zanzibarairportauthority #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DKOrqsoM8Vx/?igsh=enR0Nzc4c3BtNTRs *Sekta ya Usafiri wa Anga Zanzibar y...
Aviation Tanzania on Instagram: "Kiwanja cha Ndege cha Msalato kuanza majaribio ya kuruka na kutua ndege mwezi Juni. Majaribio ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato yanatarajiwa kuanza mwezi Juni 2025, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kukamilika kwa mradi huo mkubwa wa kimkakati unaotekelezwa jijini Dodoma. Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Abdul Mombokaleo, wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mh. Abdallah Ulega, aliyetembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho. Bw.Mombokaleo amesema Kuwa maandalizi ya hatua hiyo yako mbioni kukamilika huku ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege ukiwa umekamilika kwa 89%. Katika ziara hiyo, Waziri Ulega ameagiza taasisi mbili muhimu TAA na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kushirikiana kwa karibu na kumsimamia kwa makini Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa jengo la abiria ili kuhakikisha ubora na muda wa mradi vinazingatiwa. Ulega alionya kuwa serikali haitatoa muda wa nyongeza kwa Mkandarasi huyo na endapo atashindwa kukamilisha mradi kwa wakati, atalazimika kuilipa serikali fidia kwa kuchelewesha utekelezaji. Hadi sasa, utekelezaji wa jumla wa mradi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato umefikia 53.9% na kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha Dodoma kuwa kitovu cha biashara, uchumi, na uwekezaji nchini Tanzania. #airport #mia #msalatointernationalairport #airportauthority #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DJ9vf3OsEgZ/?igsh=MXV1MWg2N2J3ZWpsaw== *Kiwanja cha Ndege cha Msalat...
Aviation Tanzania on Instagram: "Kiwanja cha Ndege cha Saint-Tropez La Mole chafurika Maji baada ya mvua Kubwa. Uwanja wa ndege wa Saint-Tropez La Mole (LTT) umejaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kuanzia asubuhi ya Leo Mei 20,2025 na kusababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ya Ghuba ya Saint-Tropez. Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha uwanja huo ukiwa umezingirwa na maji, hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa shughuli za kawaida za usafiri wa anga katika kiwanja hicho. Mamlaka za kiwanja hicho bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu athari ya hali hiyo kwa ratiba za ndege, lakini hali hiyo inaweza kuathiri uendeshaji wa safari za anga kwa muda mfupi hadi pale itakapotengemaa. #airport #sainttropezlamoleairport #airportauthority #floods #airportinfrastructure #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DJ4JxiosdFF/?igsh=MXBwaTFndDB4dXhxcQ== *Kiwanja cha Ndege cha Saint-...