
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 22, 2025 at 05:50 PM
https://www.instagram.com/reel/DJ9vf3OsEgZ/?igsh=MXV1MWg2N2J3ZWpsaw==
*Kiwanja cha Ndege cha Msalato kuanza majaribio ya kuruka na kutua ndege mwezi Juni.*
Majaribio ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato yanatarajiwa kuanza mwezi Juni 2025, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kukamilika kwa mradi huo mkubwa wa kimkakati unaotekelezwa jijini Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Abdul Mombokaleo, wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mh. Abdallah Ulega, aliyetembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho.
Bw.Mombokaleo amesema Kuwa maandalizi ya hatua hiyo yako mbioni kukamilika huku ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege ukiwa umekamilika kwa 89%.
Katika ziara hiyo, Waziri Ulega ameagiza taasisi mbili muhimu TAA na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kushirikiana kwa karibu na kumsimamia kwa makini Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa jengo la abiria ili kuhakikisha ubora na muda wa mradi vinazingatiwa.
Ulega alionya kuwa serikali haitatoa muda wa nyongeza kwa Mkandarasi huyo na endapo atashindwa kukamilisha mradi kwa wakati, atalazimika kuilipa serikali fidia kwa kuchelewesha utekelezaji.
Hadi sasa, utekelezaji wa jumla wa mradi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato umefikia 53.9% na kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha Dodoma kuwa kitovu cha biashara, uchumi, na uwekezaji nchini Tanzania.
#airport #mia #msalatointernationalairport #airportauthority #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates