Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #aviationta

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Manusura wa ajali waishitaki Delta Airlines, wakidai fidia nyingine zaidi ya M.77 walizopewa. Abiria wawili walionusurika katika ajali ya ndege ya Delta Airlines aina ya CRJ-900 wameifungulia mashtaka kampuni ya Delta Airlines huku manusura mmoja, mwanaume kutoka Texas, akidai kuwa alipata majeraha makubwa alipokuwa "akining’iniza kichwa chini" huku "akimwagikiwa na mafuta ya ndege" wakati wajali hiyo. Bwana huyo ameandika katika madai yake, kuwa ajali hiyo imemsababishia "msongo mkubwa wa mawazo na mfadhaiko kiakili" pamoja na majeraha kwenye kichwa, shingo, mgongo, magoti na uso hivyo anastahili kupata kiasi kingine cha pesa tofauti na kiasi cha dola 30,000 (sawa na Milioni 77 za Kitanzania) ambazo zimetangazwa kutolewa kwa kila manusura wa ajali hiyo. Madai mengine yametolewa na mwanamke kutoka Minneapolis akidai kuwa alipata majeraha makubwa ya kimwili na kiakili kutokana na ajali hiyo. Mwanamama huyo ameeleza katika madai yake kuwa wahudumu wa ndege walishindwa kufuata "taratibu za msingi za kutua kwa usalama" katika uwanja wa ndege wa Toronto. Kwa mujibu wa Mkataba wa Montreal, ambao unasimamia fidia kwa abiria katika ajali za ndege kimataifa, kuna uwezekano wa kesi zaidi kufunguliwa dhidi ya Delta Air Lines. Endapo abiria wote 76 watakubali fidia iliyotangazwa na kampuni hiyo, Delta italazimika kulipa jumla ya dola milioni 2.3 (zaidi ya shilingi bilioni 7.7 za KiTanzania). Hata hivyo, madai yaliyofunguliwa yanaweza kuongeza gharama za fidia iwapo mahakama itaamua kwamba waathirika wanastahili malipo makubwa zaidi kutokana na madhara waliyoyapata. Hadi sasa, Delta haijatoa tamko rasmi kuhusu kesi hizo mpya, lakini wachambuzi wa sheria wanasema kuwa kampuni hiyo inaweza kukabiliwa na madai mengi zaidi kadri uchunguzi wa ajali hiyo unavyoendelea. . #planecrash #crj900 #toronto #deltaairlines #accident #safety #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationta"

https://www.instagram.com/p/DGYs8dctPF1/?igsh=MWszMHBydWdha2xpdA== *Manusura wa ajali waishitaki D...

Aviation Tanzania on Instagram: "Delta Airlines kuwalipa fidia ya $30,000 abiria waliopinduka na ndege Toronto. Kampuni ya ndege ya Delta Air Lines imetangaza kuwalipa fidia ya dola 30,000 kila abiria aliyekuwa ndani ya ndege iliyopata ajali na kupinduka wakati wa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pearson, Toronto, siku ya Jumatatu ya Februari 17,2025. Msemaji wa kampuni hiyo, amesema kuwa mpango wa fidia ni sehemu ya msaada wa kampuni kwa abiria waliokumbwa na ajali hiyo hiyo, akisisitiza kuwa fidia hiyo haitaathiri haki zao zozote za kisheria. Timu ya huduma ya Delta Care imekuwa ikiwasiliana na abiria ili kuwaarifu kuhusu fidia hiyo. Ndege hiyo,ilikuwa katika safari namba 4819, ilikuwa imebeba watu 80, wakiwemo abiria 76 na wafanyakazi wanne. Kufikia Jumatano asubuhi,abiria 20 kati ya abiria 21 waliokuwa wamelazwa hospitalini, walikuwa tayari wamepewa ruhusa ya kurudi nyumbani baada ya matibabu na hakuna vifo vilivyoripotiwa katika ajali hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Delta Air Lines, Ed Bastian, akizungumza na chombo cha habari cha CBS Mornings, alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikiendeshwa na kampuni tanzu ya Delta, Endeavor Air, na kuwa marubani walikuwa na uzoefu wa kutosha na mafunzo ya kukabiliana na hali yoyote. Bodi ya Usalama wa Usafiri nchini Canada (TSB) inaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Aidha, wachunguzi kutoka Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri ya Marekani (NTSB) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Shirikisho (FAA) pia wapo katika eneo la tukio kwa uchunguzi wa kina. . #planecrash #crj900 #toronto #deltaairlines #accident #safety #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationta"

https://www.instagram.com/reel/DGTSKdqtRzp/?igsh=MTV0MnM2enlya2txZg== *Delta Airlines kuwalipa fidi...

Aviation Tanzania on Instagram: "Ndege ya Delta Airlines, CRJ-900LR yapinduka,18 wajeruhiwa. Ndege ya Delta Airlines aina ya Mitsubishi CRJ-900LR, yenye namba ya usajili N12345, imepinduka wakati wa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toronto Pearson Februari 17, 2025, majira ya alasiri, na kusababisha majeraha kwa watu 18. Ndege hiyo,iliyokuwa katika safari namba 4819 ilitokea Minneapolis ikiwa na abiria 76 na wahudumu wanne. Wote waliokuwemo ndani ya ndege waliweza kuokolewa, huku 18 wakiripotiwa kujeruhiwa. Kati ya majeruhi 18, wawili walihamishiwa hospitali za dharura mjini Toronto, huku mmoja akipelekwa hospitali ya watoto kwa matibabu zaidi. Tukio hilo lilitokea majira ya mchana , muda mfupi baada ya ndege hiyo kupewa idhini ya kutua. Katika mawasiliano ya redio kati ya marubani wa ndege hiyo na mnara wa waongoza ndege (Control Tower) wa Toronto Pearson, ilionekana kuwa marubani walipewa tahadhari kuhusu mtikisiko wa hewa ulioweza kuathiri kutua kwa ndege hiyo. Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha ndege ikiwa imepinduka juu chini kwenye barabara ya kutua iliyofunikwa na theluji nzito kufuatia dhoruba kali iliyolikumba jiji la Toronto huku maafisa wa uokoaji wakifanya juhudi za kuzima moto na kuwaokoa abiria. Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) imethibitisha kuwa uchunguzi wa ajali hiyo utaongozwa na Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri ya Marekani (NTSB) kwa kushirikiana na Bodi ya Usalama wa Usafiri ya Kanada. Mtaalamu wa masuala ya usalama wa anga, John Cox, amesema kuwa ni nadra kushuhudia ndege ikipinduka baada ya kutua, hasa aina ya CRJ-900, ambayo ni ndege ya kuaminika inayoweza kuhimiri hali mbaya ya hewa. Hata hivyo, alihoji sababu ya ndege hiyo kukosa bawa lake la kulia, jambo ambalo litahitaji uchunguzi wa kina. Mkurugenzi Mtendaji wa Delta Airlines, Ed Bastian, ameeleza kuwa kampuni yake inazingatia zaidi ustawi wa walioathirika na imetoa shukrani kwa timu za uokoaji na wahudumu wa ndege hiyo kwa juhudi zao za haraka katika tukio hilo. Mashirika ya usalama wa anga yanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo. . #planecrash #crj900 #toronto #deltaairlines #accident #safety #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationta"

https://www.instagram.com/p/DGM7C-ltrvk/?igsh=bzV5MjhrNHE0cmJ3 *Ndege ya Delta Airlines, CRJ-900LR...