Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 18, 2025 at 05:14 AM
https://www.instagram.com/p/DGM7C-ltrvk/?igsh=bzV5MjhrNHE0cmJ3 *Ndege ya Delta Airlines, CRJ-900LR yapinduka,18 wajeruhiwa.* Ndege ya Delta Airlines aina ya Mitsubishi CRJ-900LR, yenye namba ya usajili N12345, imepinduka wakati wa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toronto Pearson Februari 17, 2025, majira ya alasiri, na kusababisha majeraha kwa watu 18. Ndege hiyo,iliyokuwa katika safari namba 4819 ilitokea Minneapolis ikiwa na abiria 76 na wahudumu wanne. Wote waliokuwemo ndani ya ndege waliweza kuokolewa, huku 18 wakiripotiwa kujeruhiwa. Kati ya majeruhi 18, wawili walihamishiwa hospitali za dharura mjini Toronto, huku mmoja akipelekwa hospitali ya watoto kwa matibabu zaidi. Tukio hilo lilitokea majira ya mchana , muda mfupi baada ya ndege hiyo kupewa idhini ya kutua. Katika mawasiliano ya redio kati ya marubani wa ndege hiyo na mnara wa waongoza ndege (Control Tower) wa Toronto Pearson, ilionekana kuwa marubani walipewa tahadhari kuhusu mtikisiko wa hewa ulioweza kuathiri kutua kwa ndege hiyo. Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha ndege ikiwa imepinduka juu chini kwenye barabara ya kutua iliyofunikwa na theluji nzito kufuatia dhoruba kali iliyolikumba jiji la Toronto huku maafisa wa uokoaji wakifanya juhudi za kuzima moto na kuwaokoa abiria. Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) imethibitisha kuwa uchunguzi wa ajali hiyo utaongozwa na Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri ya Marekani (NTSB) kwa kushirikiana na Bodi ya Usalama wa Usafiri ya Kanada. Mtaalamu wa masuala ya usalama wa anga, John Cox, amesema kuwa ni nadra kushuhudia ndege ikipinduka baada ya kutua, hasa aina ya CRJ-900, ambayo ni ndege ya kuaminika inayoweza kuhimiri hali mbaya ya hewa. Hata hivyo, alihoji sababu ya ndege hiyo kukosa bawa lake la kulia, jambo ambalo litahitaji uchunguzi wa kina. Mkurugenzi Mtendaji wa Delta Airlines, Ed Bastian, ameeleza kuwa kampuni yake inazingatia zaidi ustawi wa walioathirika na imetoa shukrani kwa timu za uokoaji na wahudumu wa ndege hiyo kwa juhudi zao za haraka katika tukio hilo. Mashirika ya usalama wa anga yanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo. . #planecrash #crj900 #toronto #deltaairlines #accident #safety #aircraft #aviationtanzania#aviationta

Comments