Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 22, 2025 at 07:07 PM
https://www.instagram.com/p/DGYs8dctPF1/?igsh=MWszMHBydWdha2xpdA== *Manusura wa ajali waishitaki Delta Airlines, wakidai fidia nyingine zaidi ya M.77 walizopewa.* Abiria wawili walionusurika katika ajali ya ndege ya Delta Airlines aina ya CRJ-900 wameifungulia mashtaka kampuni ya Delta Airlines huku manusura mmoja, mwanaume kutoka Texas, akidai kuwa alipata majeraha makubwa alipokuwa "akining’iniza kichwa chini" huku "akimwagikiwa na mafuta ya ndege" wakati wajali hiyo. Bwana huyo ameandika katika madai yake, kuwa ajali hiyo imemsababishia "msongo mkubwa wa mawazo na mfadhaiko kiakili" pamoja na majeraha kwenye kichwa, shingo, mgongo, magoti na uso hivyo anastahili kupata kiasi kingine cha pesa tofauti na kiasi cha dola 30,000 (sawa na Milioni 77 za Kitanzania) ambazo zimetangazwa kutolewa kwa kila manusura wa ajali hiyo. Madai mengine yametolewa na mwanamke kutoka Minneapolis akidai kuwa alipata majeraha makubwa ya kimwili na kiakili kutokana na ajali hiyo. Mwanamama huyo ameeleza katika madai yake kuwa wahudumu wa ndege walishindwa kufuata "taratibu za msingi za kutua kwa usalama" katika uwanja wa ndege wa Toronto. Kwa mujibu wa Mkataba wa Montreal, ambao unasimamia fidia kwa abiria katika ajali za ndege kimataifa, kuna uwezekano wa kesi zaidi kufunguliwa dhidi ya Delta Air Lines. Endapo abiria wote 76 watakubali fidia iliyotangazwa na kampuni hiyo, Delta italazimika kulipa jumla ya dola milioni 2.3 (zaidi ya shilingi bilioni 7.7 za KiTanzania). Hata hivyo, madai yaliyofunguliwa yanaweza kuongeza gharama za fidia iwapo mahakama itaamua kwamba waathirika wanastahili malipo makubwa zaidi kutokana na madhara waliyoyapata. Hadi sasa, Delta haijatoa tamko rasmi kuhusu kesi hizo mpya, lakini wachambuzi wa sheria wanasema kuwa kampuni hiyo inaweza kukabiliwa na madai mengi zaidi kadri uchunguzi wa ajali hiyo unavyoendelea. . #planecrash #crj900 #toronto #deltaairlines #accident #safety #aircraft #aviationtanzania#aviationta

Comments