
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 20, 2025 at 04:30 PM
https://www.instagram.com/reel/DGTSKdqtRzp/?igsh=MTV0MnM2enlya2txZg==
*Delta Airlines kuwalipa fidia ya $30,000 abiria waliopinduka na ndege Toronto.*
Kampuni ya ndege ya Delta Air Lines imetangaza kuwalipa fidia ya dola 30,000 kila abiria aliyekuwa ndani ya ndege iliyopata ajali na kupinduka wakati wa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pearson, Toronto, siku ya Jumatatu ya Februari 17,2025.
Msemaji wa kampuni hiyo, amesema kuwa mpango wa fidia ni sehemu ya msaada wa kampuni kwa abiria waliokumbwa na ajali hiyo hiyo, akisisitiza kuwa fidia hiyo haitaathiri haki zao zozote za kisheria. Timu ya huduma ya Delta Care imekuwa ikiwasiliana na abiria ili kuwaarifu kuhusu fidia hiyo.
Ndege hiyo,ilikuwa katika safari namba 4819, ilikuwa imebeba watu 80, wakiwemo abiria 76 na wafanyakazi wanne.
Kufikia Jumatano asubuhi,abiria 20 kati ya abiria 21 waliokuwa wamelazwa hospitalini, walikuwa tayari wamepewa ruhusa ya kurudi nyumbani baada ya matibabu na hakuna vifo vilivyoripotiwa katika ajali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Delta Air Lines, Ed Bastian, akizungumza na chombo cha habari cha CBS Mornings, alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikiendeshwa na kampuni tanzu ya Delta, Endeavor Air, na kuwa marubani walikuwa na uzoefu wa kutosha na mafunzo ya kukabiliana na hali yoyote.
Bodi ya Usalama wa Usafiri nchini Canada (TSB) inaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Aidha, wachunguzi kutoka Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri ya Marekani (NTSB) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Shirikisho (FAA) pia wapo katika eneo la tukio kwa uchunguzi wa kina.
.
#planecrash #crj900 #toronto #deltaairlines #accident #safety #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationta