Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #kilifair

Posts

Bank of Tanzania (BoT) on Instagram: "BENKI KUU: WATALII KURUHUSIWA KULIPA KWA FEDHA ZA KIGENI Benki Kuu ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu Kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za Mwaka 2025, ikieleza kuwa malipo ya bidhaa na huduma kati ya wakaazi na wageni, wakiwemo watalii, yanaweza kufanyika kwa kutumia fedha za kigeni. Akizungumza katika mjadala uliofanyika kwenye Maonesho ya Karibu-Kilifair jijini Arusha tarehe 8 Juni 2025, Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Akaro, alifafanua kuwa hatua hiyo inalenga kuwezesha mazingira rafiki ya kibiashara kwa wageni na urahisi wa miamala katika sekta ya utalii. “Mawakala wa utalii ambao ni wakaazi, wanaruhusiwa kutumia fedha za kigeni kulipia huduma mbalimbali zinazotolewa kwa watalii kutoka nje ya nchi,”alisema. Alisisitiza kuwa malipo yote kati ya wakaazi lazima yafanyike kwa Shilingi ya Tanzania, na ni kosa kwa mtoa huduma yeyote kukataa malipo yanayofanyika kwa kutumia Shilingi ya Tanzania. Bw. Akaro aliongeza kuwa Kanuni hizi zimetungwa kwa mujibu wa Kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, na zimeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 28 Machi 2025. “Tangu kuanza kutumika kwa kanuni hizo, kumekuwa na matokeo chanya ikiwemo kuongezeka kwa ukwasi wa fedha za kigeni. Kwa mfano, miamala ya Dola za Marekani kwenye soko la fedha za kigeni la rejareja nchini imeongezeka kutoka wastani wa dola milioni 40 hadi milioni 69 kwa siku”, alisema. Vilevile, alibainisha kuwa, kutokana na kuongezeka kwa ukwasi wa fedha za kigeni, thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani imeimarika kwa kiwango kikubwa, na matarajio ni kwamba itaendelea kuimarika zaidi. “Hii ni kutokana na kuanza kwa msimu wa mapato ya fedha za kigeni, hususan kutoka kwenye sekta kama utalii, kilimo na mauzo ya bidhaa nje ya nchi, ambazo kwa kawaida huingiza fedha nyingi za kigeni katika kipindi hiki,”alisema. Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu utekelezaji wa kanuni hizi, ili kuhakikisha kwamba zinazingatiwa kwa manufaa ya uchumi wa taifa na ustawi wa sekta za kibiashara, hasa utalii."

BENKI KUU: WATALII KURUHUSIWA KULIPA KWA FEDHA ZA KIGENI Benki Kuu ya Tanzania imetoa ufafanuzi ku...

Aviation Tanzania on Instagram: "Aviation Tanzania Network, tumepata fursa ya kutembelea katika maonyesho ya Karibu Kilifair 2025 jijini Arusha, tukiangazia zaidi ushiriki wa watoaji wa huduma ya usafiri wa anga katika maonyesho hayo ambayo yamehitimishwa hii Leo Juni 8,2025. Maonyesho haya yaliyoanza Juni 6,2025 yamefanyika Kwa Lengo la kukuza zaidi sekta ya utalii na biashara yakihudhuriwa na zaidi ya kampuni 500 toka nchi mbalimbali Africa Mashariki. @flightlinktz @precisionairtz @flyboskies #kilifair #kilifair2025 #exhibition #airlines #aviationtanzania✈ #aviatamedia"

https://www.instagram.com/p/DKpi1j-NKaw/?igsh=aG9xMzlzemFzN2R1 Aviation Tanzania Network, tumepata ...

Aviation Tanzania on Instagram: "Katika maonyesho ya @kilifair 2025, Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la @flightlinktz , @munawerdhirani ameeleza namna shirika hilo lilivyojipanga kuongeza safari za ndani na nje ya nchi. Safari hizo ni pamoja na zile kati ya Uwanja wa Ndege wa Arusha na uwanja wa ndege wa Wilson zitakazozinduliwa tarehe 15 Juni 2025, pamoja na safari kati ya Zanzibar na Jomo Kenyatta zitakazoanza tarehe 1 Julai 2025. Aidha, Flightlink imepanga kuanzisha safari kati ya Mwanza na Kilimanjaro, zitakazozinduliwa ndani ya mwezi Julai. #Airlines #routeexpansion #flightlink #aviationlovers #aviationcareer #atr72500 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKoSH0Pt-2f/?igsh=MTd5YnNsd204dnNyZw== *Flightlink yapanga kuanzisha...

Aviation Tanzania on Instagram: "Flightlink yashiriki katika maonyesho ya Karibu Kilifair Arusha. Shirika la ndege la @flightlinktz , limeshiriki katika maonyesho ya kibiashara na Utalii ya Karibu Kilifair Kwa mwaka 2025. Maonyesho hayo yaliyozinduliwa siku ya Jana Juni 6,2025 yalihudhuriwa na mgeni rasmi, Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh.Dotto Biteko, yanafanyika katika viwanja vya Magereza jijini Arusha na yanatarajia kuhitimishwa siku ya kesho Juni 08,2025. Zaidi ya makampuni 500 kutoka Afrika mashariki yamepata fursa ya kuonyesha bidhaa na huduma zao katika maonyesho hayo Kwa mwaka huu, maonyesho ambayo yanatazamiwa kukuza zaidi sekta ya utalii wa ndani na nje ya nchi. Flightlink imepata fursa ya kuonyesha na kutangaza zaidi huduma ya safari zake ikiwemo safari mpya zinazotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni zikiwemo safari za ndani na nje ya nchi. Endelea kutufuatilia Kwa habari mbalimbali kuhusu maonyesho ya Karibu Kilifair 2025. #exhibition #airline #flightlink #newroutes #routeexpansion #ys #kilifair2025 #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"

https://www.instagram.com/p/DKm9B4wNwpQ/?igsh=MWhubHIxdXJnM2M3NQ== *Flightlink yashiriki katika mao...

NCAA TUPO KARIBU-KILIFAIR 2025, KARIBU TUKUHUDUMIE...

NCAA TUPO KARIBU-KILIFAIR 2025, KARIBU TUKUHUDUMIE.

The Wait Is Over, KARIBU-KILIFAIR 2025 Begins Today – Go Places Digital

https://goplacesdigital.com/the-wait-is-over-karibu-kilifair-2025-begins-today/ 🌍 *Day 1 Buzz from ...

Bank of Tanzania (BoT) on Instagram: "Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeungana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kushiriki Maonesho ya Utalii ya Karibu-Kilifair 2025, yanayofanyika katika viwanja vya Magereza, jijini Arusha kuanzia tarehe 06 hadi 08 Juni. Kupitia ushiriki huu, Benki Kuu inatumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ya msingi katika kusimamia uchumi nchini. Katika maonesho hayo, Benki Kuu imeweka msisitizo maalum kwenye Kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za Mwaka 2025, ambazo zinalenga kuimarisha uthabiti wa thamani ya Shilingi ya Tanzania ili kuchochea maendeleo endelevu ya uchumi na kuhakikisha ustawi wa taifa kwa ujumla."

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeungana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kushiriki Maonesho ya U...

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. D...

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amefungua Maonesho ya Utalii ya...

Secure Your Spot At KARIBU-KILIFAIR 2025 Today – Go Places Digital

https://goplacesdigital.com/secure-your-spot-at-karibu-kilifair-2025-today/ 🌍✈️ #ConnectWithBuyers ...

Expand, Connect, And Thrive At KARIBU-KILIFAIR 2025 In Arusha - Go Places Digital

https://goplacesdigital.com/expand-connect-and-thrive-at-karibu-kilifair-2025-in-arusha/ 🌍✨ Karibu-...

The Countdown Is On, Register For KARIBU-KILIFAIR 2025 & Elevate Your Business - Go Places™ Digital

https://goplacesdigital.com/the-countdown-is-on-register-for-karibu-kilifair-2025-elevate-your-busin...

KARIBU-KILIFAIR 2025, Register Now & Connect With 500+ Global Buyers - Go Places Digital

https://goplacesdigital.com/karibu-kilifair-2025-register-now-connect-with-500-global-buyers/ 🌍✨ Ge...