Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #precisionair
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Precision Air yatembelea Kituo cha watoto Cornel Ngaleku, kumuenzi muanzilishi wa Shirika hilo. Shirika la ndege la @precisionairtz limepata fursa ya kutembelea Kituo cha Watoto cha Cornel Ngaleku na kutoa msaada wao wa upendo kwa watoto waliopo kituoni hapo. Kupitia ujumbe wake rasmi, shirika hilo limeeleza kuwa, ziara hiyo pia imefanyika Kama namna ya kumuenzi mwanzilishi wa shirika hilo, marehemu Michael Shirima, ambaye ndoto na maono yake bado yanaendelea kuwa dira ya huduma na mshikamano wa kijamii. Kupitia tukio hilo, Precision Air imeeleza kuguswa na furaha iliyosambaa kwenye nyuso za watoto hao, jambo linalothibitisha nguvu ya huruma na mshikamano wa jamii. #Airlines #pw #precisionair #youarewhywefly #aviationlovers #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DK2aM52tiI9/?igsh=MncyMDFtYjBhMzd1 *Precision Air yatembelea Kituo cha ...
Aviation Tanzania on Instagram: "Precision Air yatangaza kuanza muhula mpya wa mafunzo ya uhudumu wa ndege mwezi Juni. Shirika la ndege la @precisionairtz limetangaza kuanza rasmi muhula mpya wa kozi za wahudumu wa ndege (Cabin Crew) kuanzia Juni 16, 2025, ikiwa ni baada ya awamu ya 13 ya wahudumu wa ndege kuhitimu masomo yao Mei 30, 2025. Wahudumu waliohitimu wamepitia mafunzo ya kina yaliyowajengea uwezo katika maeneo mbalimbali kama vile taratibu za usalama wa abiria, huduma kwa wateja, mawasiliano bora na ujuzi mwingine muhimu unaowasaidia kuwa tayari kwa soko la ajira ndani na nje ya nchi. Kwa taarifa zaidi juu ya namna ya kujiunga na mafunzo haya, tembelea tovuti yao [www.precisionairtz.com](http://www.precisionairtz.com) au piga simu kupitia namba 0787 006 766. #cabincrew #airline #precisionair #pw #youarewhywefly #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DKTsdF4MpAj/?igsh=aGtnajExZmprNGZs *Precision Air yatangaza kuanza muhu...
Aviation Tanzania on Instagram: "Precision Air’s ATR 42-500, with registration number 5H-PWE, departing from Julius Nyerere International Airport. #airline #precisionair #pw #youarewhywefly #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DKHC8mXswO4/?igsh=MTUyeWthaDNvZzNmZQ== *Precision Air ATR 42-500 Dep...
Aviation Tanzania on Instagram: "Zimesalia siku 3, Precision Air itue kwa mara ya kwanza katika mji wa Iringa. Shirika la ndege la @precisionairtz lipo mbioni kuanza rasmi safari zake za anga kati ya Dar es Salaam na Iringa kuanzia tarehe 3 Machi 2025. Huduma hii mpya inalenga kuboresha upatikanaji wa usafiri wa anga nchini Tanzania, kupunguza muda wa safari, na kutoa chaguo la usafiri bora,hakika na nafuu kwa wakazi wa Iringa na maeneo jirani. Precision Air itaunganisha abiria kati ya Dar es Salaam, Dodoma, na Iringa mara tatu kwa wiki (Jumatatu, Jumatano, Ijumaa). Gharama ya safari:Safari ya kwenda: Sh. 99,000, Safari ya kwenda na kurudi: Sh.190,000 Precision Air Services ilianzishwa mwaka 1993 kama kampuni ya usafiri wa anga ya kibinafsi iliyotoahuduma ya ndege za kukodi, ikitoa huduma hasa kwa watalii waliotembelea vivutio vya asili vya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kreta ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania, Kisiwa cha Zanzibar katika Bahari ya Hindi, na sehemu nyingine za nchi kutoka mji wa Arusha kama kituo chake kikuu. Kwa sasa, makao makuu yake yapo jijini Dar es Salaam, na imekua na kuwa shirika la ndege lenye sifa kubwa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Shirika hili linafanya safari kutoka mji wa Dar es Salaam kwenda Arusha, Bukoba, Kilimanjaro, Kahama, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar, Seronera, Nairobi, na Entebbe. #Airlines #precisionair #youarewhywefly #avgeek #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"
https://www.instagram.com/p/DGk7vOWtYBb/?igsh=MXYybDhoZ2Ywemp1Zw== *Zimesalia siku 3, Precision Air...