Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 13, 2025 at 05:58 PM
https://www.instagram.com/p/DK2aM52tiI9/?igsh=MncyMDFtYjBhMzd1 *Precision Air yatembelea Kituo cha watoto Cornel Ngaleku, kumuenzi muanzilishi wa Shirika hilo.* Shirika la ndege la @precisionairtz limepata fursa ya kutembelea Kituo cha Watoto cha Cornel Ngaleku na kutoa msaada wao wa upendo kwa watoto waliopo kituoni hapo. Kupitia ujumbe wake rasmi, shirika hilo limeeleza kuwa, ziara hiyo pia imefanyika Kama namna ya kumuenzi mwanzilishi wa shirika hilo, marehemu Michael Shirima, ambaye ndoto na maono yake bado yanaendelea kuwa dira ya huduma na mshikamano wa kijamii. Kupitia tukio hilo, Precision Air imeeleza kuguswa na furaha iliyosambaa kwenye nyuso za watoto hao, jambo linalothibitisha nguvu ya huruma na mshikamano wa jamii. #airlines #pw #precisionair #youarewhywefly #aviationlovers #aviationcareer #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments