
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 31, 2025 at 06:27 AM
https://www.instagram.com/p/DKTsdF4MpAj/?igsh=aGtnajExZmprNGZs
*Precision Air yatangaza kuanza muhula mpya wa mafunzo ya uhudumu wa ndege mwezi Juni.*
Shirika la ndege la @precisionairtz limetangaza kuanza rasmi muhula mpya wa kozi za wahudumu wa ndege (Cabin Crew) kuanzia Juni 16, 2025, ikiwa ni baada ya awamu ya 13 ya wahudumu wa ndege kuhitimu masomo yao Mei 30, 2025.
Wahudumu waliohitimu wamepitia mafunzo ya kina yaliyowajengea uwezo katika maeneo mbalimbali kama vile taratibu za usalama wa abiria, huduma kwa wateja, mawasiliano bora na ujuzi mwingine muhimu unaowasaidia kuwa tayari kwa soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Kwa taarifa zaidi juu ya namna ya kujiunga na mafunzo haya, tembelea tovuti yao [www.precisionairtz.com](http://www.precisionairtz.com) au piga simu kupitia namba 0787 006 766.
#cabincrew #airline #precisionair #pw #youarewhywefly #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates