
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 27, 2025 at 01:03 PM
https://www.instagram.com/p/DGk7vOWtYBb/?igsh=MXYybDhoZ2Ywemp1Zw==
*Zimesalia siku 3, Precision Air itue kwa mara ya kwanza katika mji wa Iringa.*
Shirika la ndege la @precisionairtz lipo mbioni kuanza rasmi safari zake za anga kati ya Dar es Salaam na Iringa kuanzia tarehe 3 Machi 2025.
Huduma hii mpya inalenga kuboresha upatikanaji wa usafiri wa anga nchini Tanzania, kupunguza muda wa safari, na kutoa chaguo la usafiri bora,hakika na nafuu kwa wakazi wa Iringa na maeneo jirani.
Precision Air itaunganisha abiria kati ya Dar es Salaam, Dodoma, na Iringa mara tatu kwa wiki (Jumatatu, Jumatano, Ijumaa).
Gharama ya safari:Safari ya kwenda: Sh. 99,000, Safari ya kwenda na kurudi: Sh.190,000
Precision Air Services ilianzishwa mwaka 1993 kama kampuni ya usafiri wa anga ya kibinafsi iliyotoahuduma ya ndege za kukodi, ikitoa huduma hasa kwa watalii waliotembelea vivutio vya asili vya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kreta ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania, Kisiwa cha Zanzibar katika Bahari ya Hindi, na sehemu nyingine za nchi kutoka mji wa Arusha kama kituo chake kikuu.
Kwa sasa, makao makuu yake yapo jijini Dar es Salaam, na imekua na kuwa shirika la ndege lenye sifa kubwa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Shirika hili linafanya safari kutoka mji wa Dar es Salaam kwenda Arusha, Bukoba, Kilimanjaro, Kahama, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar, Seronera, Nairobi, na Entebbe.
#airlines #precisionair #youarewhywefly #avgeek #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈