Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #womeninaviation
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Gökçe Kübra, rubani wa kwanza wa kike kuwa Captain wa A380, ndege kubwa zaidi ya abiria. Gökçe Kübra Yıldırım kutoka nchini Uturuki ameweka historia kwa kuwa rubani wa kwanza wa kike kuwa rubani kiongozi (Captain) Airbus A380, ndege kubwa zaidi ya abiria duniani. Baada ya miaka kadhaa kama rubani msaidizi, Gökçe sasa amepandishwa cheo na kupewa majukumu ya kuiongoza A380 katika shirika la ndege la Emirates lenye makao yake nchini Dubai. Safari yake katika anga aliianza kama mwanafunzi wa mafunzo katika kitengo cha matengenezo cha shirika la ndege la Turkish Airlines kinachofahamika kama THY Teknik, Baada ya kukamilisha mafunzo yake, alijiunga na shirika hilo kama rubani msaidizi wa ndege za Airbus, akipata uzoefu mkubwa katika sekta ya anga kibiashara. Bqadaye,Gökçe alihamia katika shirika la ndege la Dubai, ambako aliendelea kurusha Airbus A380. Hatimaye, kupitia jitihada na uzoefu wa miaka mingi, amefanikisha hatua ya kuwa Captain wa ndege hiyo kubwa, akivunja rekodi kwa wanawake katika anga. Captain Gökçe Aliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa safari yake ya takriban miaka 12 imekuwa na changamoto na mafanikio ambayo yamemjenga. Alieleza kuwa kazi ya urubani si tu ajira kwake, bali ni sehemu ya maisha yake. Mafanikio yake yanatoa hamasa kwa wanawake wanaotamani kuingia kwenye fani ya urubani, yakionyesha kuwa kwa bidii na uvumilivu, hakuna ndoto isiyowezekana. . #womeninaviation #emiratesairline #aviationcareer #aviation #dreamliner #aviatamedia #aviationtanzania"
https://www.instagram.com/p/DGkqZ0DN41Z/?igsh=MXNqeW45aWFqb2M5cA== *Gökçe Kübra, rubani wa kwanza w...
Aviation Tanzania on Instagram: "Captain Irene Koki Mutungi, mwanamama mwenye historia ya kipekee katika sekta ya anga barani Afrika kwa kuwa ndiye rubani wa kwanza mwanamke barani Afrika kuendesha ndege ya aina ya Boeing 787 Dreamliner. Alizaliwa mwaka 1976 nchini Kenya, ambapo baba yake alikuwa rubani mwenye leseni ya kuendesha ndege za biashara (Commercial Pilot Licence) akifanya kazi na shirika la ndege la Kenya Airways. Koki alisoma katika shule ya Moi Girls iliyopo nchini Nairobi, na baada ya kumaliza elimu ya sekondari mwaka 1992 akiwa na miaka 17, alianza kujifunza urubani. Safari yake ya anga ilianza katika shule ya Wilson Airport nchini Nairobi, ambapo alihitimu na kupata leseni ya kuendesha ndege binafsi (Private Pilot Licence). Aliendelea na mafunzo ya urubani katika mji wa Oklahoma nchini Marekani, ambapo alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege za biashara kutoka Mamlaka ya anga nchini Marekani, FAA. Mwaka 1995, Koki alirejea Kenya na kuajiriwa katika shirika la ndege la Kenya Airways, akiwa mwanamke wa kwanza rubani katika taifa hilo. Alidumu katika rekodi hii kwa miaka sita kabla ya Kenya kupata rubani mwingine mwanamke. Mwaka 2004, Irene alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege kubwa za abiria, na kuwa rubani wa kwanza wa kike Afrika kupata leseni hiyo. Koki alirusha ndege za aina mbalimbali, zikiwemo Boeing 737 hadi Boeing 767. Hatimaye, alikamilisha mafunzo yake na kufuzu kuendesha ndege za Dreamliner, na Aprili 15, 2014, waajiri wake walimtangaza kama mwanamke wa kwanza kuwahi kuendesha Dreamliner barani Afrika. Mwaka 2014, aliandika historia kwa kufuzu kuwa Captain wa ndege hiyo ya kisasa. Captain Irene anajulikana pia kwa mchango wake katika kutoa mwongozo na kuwahamasisha marubani wachanga, hasa wanawake wanaotamani kuingia katika fani hii. Kutokana na mafanikio yake makubwa, Captain Koki amepokea tuzo nyingi za kutambua mchango wake katika sekta ya anga. Umahiri wake ulimfanya atambuliwe na CNN kama mmoja wa viongozi wanaochochea mabadiliko barani Afrika, heshima inayodhihirisha athari chanya ya safari yake ya urubani. @flygirl_koki @officialkenyaairways #womeninaviation #kenyaairways #aviationcareer #aviation #dreamliner #aviatamedia #aviationtanzania"
https://www.instagram.com/p/DGdKJTRNHee/?igsh=MWZmang4MTFlMXR1aQ== *Huyu ndiye, Rubani wa Kwanza mw...
Mapema mwezi uliopita, tulikuletea mahojiano maalu...
Mapema mwezi uliopita, tulikuletea mahojiano maalum na mmoja wa wanufaika wa Mfuko wa Mafunzo ya Uru...