
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 24, 2025 at 12:31 PM
https://www.instagram.com/p/DGdKJTRNHee/?igsh=MWZmang4MTFlMXR1aQ==
*Huyu ndiye, Rubani wa Kwanza mwanamke Afrika kurusha Ndege za Dreamliner*
Captain Irene Koki Mutungi, mwanamama mwenye historia ya kipekee katika sekta ya anga barani Afrika kwa kuwa ndiye rubani wa kwanza mwanamke barani Afrika kuendesha ndege ya aina ya Boeing 787 Dreamliner.
Alizaliwa mwaka 1976 nchini Kenya, ambapo baba yake alikuwa rubani mwenye leseni ya kuendesha ndege za biashara (Commercial Pilot Licence) akifanya kazi na shirika la ndege la Kenya Airways. Koki alisoma katika shule ya Moi Girls iliyopo nchini Nairobi, na baada ya kumaliza elimu ya sekondari mwaka 1992 akiwa na miaka 17, alianza kujifunza urubani.
Safari yake ya anga ilianza katika shule ya Wilson Airport nchini Nairobi, ambapo alihitimu na kupata leseni ya kuendesha ndege binafsi (Private Pilot Licence). Aliendelea na mafunzo ya urubani katika mji wa Oklahoma nchini Marekani, ambapo alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege za biashara kutoka Mamlaka ya anga nchini Marekani, FAA.
Mwaka 1995, Koki alirejea Kenya na kuajiriwa katika shirika la ndege la Kenya Airways, akiwa mwanamke wa kwanza rubani katika taifa hilo. Alidumu katika rekodi hii kwa miaka sita kabla ya Kenya kupata rubani mwingine mwanamke. Mwaka 2004, Irene alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege kubwa za abiria, na kuwa rubani wa kwanza wa kike Afrika kupata leseni hiyo.
Koki alirusha ndege za aina mbalimbali, zikiwemo Boeing 737 hadi Boeing 767. Hatimaye, alikamilisha mafunzo yake na kufuzu kuendesha ndege za Dreamliner, na Aprili 15, 2014, waajiri wake walimtangaza kama mwanamke wa kwanza kuwahi kuendesha Dreamliner barani Afrika. Mwaka 2014, aliandika historia kwa kufuzu kuwa Captain wa ndege hiyo ya kisasa.
Captain Irene anajulikana pia kwa mchango wake katika kutoa mwongozo na kuwahamasisha marubani wachanga, hasa wanawake wanaotamani kuingia katika fani hii.
Kutokana na mafanikio yake makubwa, Captain Koki amepokea tuzo nyingi za kutambua mchango wake katika sekta ya anga. Umahiri wake ulimfanya atambuliwe na CNN kama mmoja wa viongozi wanaochochea mabadiliko barani Afrika, heshima inayodhihirisha athari chanya ya safari yake ya urubani.
@flygirl_koki @officialkenyaairways
#womeninaviation #kenyaairways #aviationcareer #aviation #dreamliner #aviatamedia #aviationtanzania