Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 27, 2025 at 10:27 AM
https://www.instagram.com/p/DGkqZ0DN41Z/?igsh=MXNqeW45aWFqb2M5cA== *Gökçe Kübra, rubani wa kwanza wa kike kuwa Captain wa A380, ndege kubwa zaidi ya abiria.* Gökçe Kübra Yıldırım kutoka nchini Uturuki ameweka historia kwa kuwa rubani wa kwanza wa kike kuwa rubani kiongozi (Captain) Airbus A380, ndege kubwa zaidi ya abiria duniani. Baada ya miaka kadhaa kama rubani msaidizi, Gökçe sasa amepandishwa cheo na kupewa majukumu ya kuiongoza A380 katika shirika la ndege la Emirates lenye makao yake nchini Dubai. Safari yake katika anga aliianza kama mwanafunzi wa mafunzo katika kitengo cha matengenezo cha shirika la ndege la Turkish Airlines kinachofahamika kama THY Teknik, Baada ya kukamilisha mafunzo yake, alijiunga na shirika hilo kama rubani msaidizi wa ndege za Airbus, akipata uzoefu mkubwa katika sekta ya anga kibiashara. Bqadaye,Gökçe alihamia katika shirika la ndege la Dubai, ambako aliendelea kurusha Airbus A380. Hatimaye, kupitia jitihada na uzoefu wa miaka mingi, amefanikisha hatua ya kuwa Captain wa ndege hiyo kubwa, akivunja rekodi kwa wanawake katika anga. Captain Gökçe Aliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa safari yake ya takriban miaka 12 imekuwa na changamoto na mafanikio ambayo yamemjenga. Alieleza kuwa kazi ya urubani si tu ajira kwake, bali ni sehemu ya maisha yake. Mafanikio yake yanatoa hamasa kwa wanawake wanaotamani kuingia kwenye fani ya urubani, yakionyesha kuwa kwa bidii na uvumilivu, hakuna ndoto isiyowezekana. . #womeninaviation #emiratesairline #aviationcareer #aviation #dreamliner #aviatamedia #aviationtanzania

Comments