Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 12, 2025 at 06:19 PM
https://www.instagram.com/p/DF-4KnrtAzp/?igsh=M3cxd2hyMHU2eTBq *DRC yapiga marufuku ndege zote za Rwanda kupita kwenye anga lake, Kufuatia Mgogoro wa waasi wa M23.* Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imepiga marufuku ndege zote zilizosajiliwa nchini Rwanda kupita katika anga lake kwa muda wa miezi mitatu kutokana na mgogoro unaoendelea nchini Kongo unaohusisha kundi la waasi wa M23. Taarifa iliyotolewa kwa wanaanga Notice to Airmen (NOTAM) hii leo,imeeleza kuwa, ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa au zenye makao yake nchini Rwanda zimezuiwa kuruka katika anga la DRC au kutua nchini humo huku marufuku hii ikidumu hadi ifikapo Mei 11 kwa sababu za kiusalama. Serikali ya DRC imechukua uamuzi huu baada ya mazungumzo ya amani yaliyofanyika kwa lengo la kumaliza mapigano kutofanikiwa. Katika wiki za hivi karibuni, waasi wa M23 wameanzisha mashambulizi mapya mashariki mwa DRC huku Serikali ya Kongo ikiituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi na inadai kwamba wanajeshi wa Rwanda walioko ndani ya ardhi yake waondoke.Hata hivyo, Rwanda imekanusha madai hayo. Umoja wa mataifa umeripokuwa, mgogoro huu umesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000, majeruhi 2,880, na zaidi ya watu 500,000 kuyakimbia makazi yao tangu Januari 26.Hii inaongeza idadi ya wakimbizi wa ndani kufikia milioni 6.4 nchini humo. Licha ya waasi wa M23 kutangaza usitishaji wa mapigano Februari 4, vita bado vinaendelea. Kundi hilo, ambalo liliiteka Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini mwishoni mwa Januari, linadai kuwa limeunda utawala wake ndani ya mji huo. Mapigano hayo pia yameathiri vikosi vya kulinda amani vya kimataifa, ambapo walinda amani 20, wakiwemo 14 kutoka Afrika Kusini, wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni. Miili ya wanajeshi wa Afrika Kusini waliouawa inatarajiwa kurejeshwa nyumbani siku ya Alhamisi. Serikali ya DRC inasisitiza kuwa Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 na kwamba imetuma wanajeshi mashariki mwa Kongo tangu mashambulizi ya hivi karibuni yalipoanza, madai ambayo Kigali inaendelea kuyakanusha. . #rwandaair #m23 #aviatamedia #aviationtanzaniaupdates #aviata

Comments