Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #aviatamedia

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Mashirika ya Ndege 46 na Wajumbe 500 Wakutana Katika Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Zanzibar. Zaidi ya mashirika ya ndege 46 na wajumbe 500 kutoka mataifa mbalimbali duniani wamekutana visiwani Zanzibar kushiriki Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Afrika (AviaDev Africa), unaofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip. Mkutano huu umezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni mgeni rasmi wa tukio hilo ukiwakutanisha Wakurugenzi Wakuu wa mashirika ya ndege, viongozi wa viwanja vya ndege, maafisa wa bodi za utalii, na wawakilishi wa serikali kutoka Afrika na kwingineko duniani. Mkutano huo umetajwa kusaidia ongezeko la safari za moja kwa moja visiwani Zanzibar na maeneo mengine ya Afrika kwa njia ya ushirikiano wa kimkakati kati ya sekta binafsi na serikali, ili kuchochea ukuaji wa utalii na uchumi wa ndani. Mkutano huo unajumuisha majadiliano ya ana kwa ana baina ya mashirika ya ndege na viwanja vya ndege, mijadala ya kitaalamu kuhusu usafiri wa anga, pamoja na maonyesho ya fursa za uwekezaji. #aviadev #aviation #aviationprofessionals #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviatamedia"

https://www.instagram.com/p/DKy67lktNC1/?igsh=MWZ2dWUyeTJoYWRpcQ== *Mashirika ya Ndege 46 na Wajumb...

Aviation Tanzania on Instagram: "Aviation Tanzania Network, tumepata fursa ya kutembelea katika maonyesho ya Karibu Kilifair 2025 jijini Arusha, tukiangazia zaidi ushiriki wa watoaji wa huduma ya usafiri wa anga katika maonyesho hayo ambayo yamehitimishwa hii Leo Juni 8,2025. Maonyesho haya yaliyoanza Juni 6,2025 yamefanyika Kwa Lengo la kukuza zaidi sekta ya utalii na biashara yakihudhuriwa na zaidi ya kampuni 500 toka nchi mbalimbali Africa Mashariki. @flightlinktz @precisionairtz @flyboskies #kilifair #kilifair2025 #exhibition #airlines #aviationtanzania✈ #aviatamedia"

https://www.instagram.com/p/DKpi1j-NKaw/?igsh=aG9xMzlzemFzN2R1 Aviation Tanzania Network, tumepata ...

Aviation Tanzania on Instagram: "United Airlines Yaanzisha Safari Yake ya Sita Afrika: Washington–Dakar. Shirika la ndege la @united limeanzisha safari mpya ya moja kwa moja kutoka Washington, D.C. kwenda Dakar, Senegal. Hii ni safari ya sita barani Afrika huku safari nyingine tayari zinafanyika kutoka Washington hadi miji ya Cape Town na Johannesburg nchini Afrika Kusini, Accra nchini Ghana, Lagos nchini Nigeria, na Marrakesh nchini Morocco. Safari ya kwanza ya kuelekea Dakar, ilikuwa na jumla abiria 505, jambo linaloonesha uhitaji mkubwa wa huduma hii ya usafiri wa anga katika miji hiyo. #routeexpansion #airline #unitedairlines #africanflights #dakar #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviatamedia"

https://www.instagram.com/reel/DKUlglSsXFh/?igsh=aXpvZGwzemZ2NzF4 *United Airlines Yaanzisha Safari...

Aviation Tanzania on Instagram: "Small Plane Makes Emergency Belly Landing in Texas. A pilot made an emergency belly landing on a foam-covered runway at an airport in Arlington, Texas on Thursday after reporting equipment issues. According to the Federal Aviation Administration (FAA), there were two people onboard the small aircraft at the time. No injuries have been reported. Emergency crews responded by covering the runway with foam as a safety precaution before the landing. #bellylanding #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"

https://www.instagram.com/reel/DKAass2spCn/?igsh=MTUzMXFqeDhuYWVqOA== *Small Plane Makes Emergency ...

Aviation Tanzania on Instagram: "Ndege ya Jeshi la anga la Morocco, F-16 ikijaza mafuta angani Katika Mazoezi ya Kivita na Marekani. Tazama ndege ya kivita aina ya F-16 ya Jeshi la Anga la Morocco ikijaza mafuta angani kutoka kwenye ndege ya Jeshi la Anga la Marekani, ya KC-135 ya wakati wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayoendelea nchini Morocco. Zoezi hilo ni sehemu ya mafunzo ya African Lion, ambayo yanaendelea hadi Mei 23,2025 yakilenga kufanyia mazoezi ujuzi wa kujaza mafuta angani katika mazingira ya kivita. #africanlionexcercise #f16 #kc135 #airrefueling #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"

https://www.instagram.com/reel/DJ3W9v8MIJg/?igsh=b2Z6c3B3am0zZTJ3 *Ndege ya Jeshi la anga la Morocc...

Aviation Tanzania on Instagram: "Katika safari za ndege, ulevi uliopitiliza kwa abiria unaweza kusababisha changamoto mbalimbali, ikiwemo usumbufu kwa wasafiri wengine na kuhatarisha usalama baadhi ya abiria waliopo ndani ya ndege. @dr.nasranassor, daktari wa wanaanga nchini, ameeleza kuhusu sheria za anga zinazohusu abiria wenye tabia zisizofaa safarini. Amebainisha kuwa abiria mlevi anayesababisha usumbufu na kero kwa wengine haruhusiwi kupanda ndege. Hata hivyo, abiria mwenye kiwango kidogo cha ulevi anaweza kuendelea na safari mradi hatosababisha usumbufu kwa wengine. Tazama mahojiano haya kamili kwenye YouTube channel yetu, Aviation Tanzania, kwa kubonyeza kiungo kilichopo kwenye bio. #aviationmedicine #cabincrew #aviationcareer #aviation #aviationlovers #aviatamedia #aviationtanzaniaupdates #AviationTanzania✈"

https://www.instagram.com/reel/DGnqo16NENc/?igsh=ZDVsbG15eWo1aDBn Katika safari za ndege, ulevi uli...

Aviation Tanzania on Instagram: "Dubai yajenga uwanja wa ndege mkubwa zaidi duniani, utakaohudumia abiria milioni 260. Dubai inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa zaidi duniani,unaojulikana kama uwanja wa ndege wa kimataifa wa Al Maktoum, ikiwa imewekeza kiasi cha dola za kimarekani bilioni 35. Mradi huu wa kisasa uliodhinishwa Aprili 2024 na mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid al-Maktoum,unajumuisha ujenzi wa jengo jipya la abiria, ambalo pia linajulikana kama Dubai World Central, sambamba na ujenzi wa njia tano za ndege (runways), kila moja ikiwa na urefu wa kilomita 4.5, ili kuruhusu ndege kuruka na kutua kwa wakati mmoja. Vilevile ujenzi wa njia zinazoelekea katika eneo la kupaki magari ambazo zitasaidia kupunguza msongamano na kuboresha muda wa mzunguko wa ndege. Aidha, vituo viwili vya uongozaji wa ndege (Air Traffic control) vitajengwa katika teknolojia ya kisasa, ili kuhakikisha usalama na ufanisi wa shughuli za anga. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Al Maktoum utakapo kamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 260 kila mwaka, ambayo ni mara tano zaidi kuliko uwezo wa sasa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai (DXB). Vilevile, utakapomalizika uwanja huo, Shughuli zote za ndege kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai (DXB) zitahamia kwenye Uwanja huo ifikapo mwaka 2035. Mradi huu unalenga kudumisha nafasi ya nchi ya Dubai kama kitovu cha kimataifa cha usafiri wa anga na kuweka mazingira bora kwa shughuli za anga za siku zijazo. . #dxb #dubai #almakhtoumairport #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata"

https://www.instagram.com/p/DGm2UjptyLi/?igsh=dnNubmc2Y3M4N3U0 *Dubai yajenga uwanja wa ndege mkub...

*Embraer delays E175-E2 to 2027, due to U.S. Pilot...

*Embraer delays E175-E2 to 2027, due to U.S. Pilot union rules.* Embraer has announced a further fo...

Aviation Tanzania on Instagram: "Gökçe Kübra, rubani wa kwanza wa kike kuwa Captain wa A380, ndege kubwa zaidi ya abiria. Gökçe Kübra Yıldırım kutoka nchini Uturuki ameweka historia kwa kuwa rubani wa kwanza wa kike kuwa rubani kiongozi (Captain) Airbus A380, ndege kubwa zaidi ya abiria duniani. Baada ya miaka kadhaa kama rubani msaidizi, Gökçe sasa amepandishwa cheo na kupewa majukumu ya kuiongoza A380 katika shirika la ndege la Emirates lenye makao yake nchini Dubai. Safari yake katika anga aliianza kama mwanafunzi wa mafunzo katika kitengo cha matengenezo cha shirika la ndege la Turkish Airlines kinachofahamika kama THY Teknik, Baada ya kukamilisha mafunzo yake, alijiunga na shirika hilo kama rubani msaidizi wa ndege za Airbus, akipata uzoefu mkubwa katika sekta ya anga kibiashara. Bqadaye,Gökçe alihamia katika shirika la ndege la Dubai, ambako aliendelea kurusha Airbus A380. Hatimaye, kupitia jitihada na uzoefu wa miaka mingi, amefanikisha hatua ya kuwa Captain wa ndege hiyo kubwa, akivunja rekodi kwa wanawake katika anga. Captain Gökçe Aliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa safari yake ya takriban miaka 12 imekuwa na changamoto na mafanikio ambayo yamemjenga. Alieleza kuwa kazi ya urubani si tu ajira kwake, bali ni sehemu ya maisha yake. Mafanikio yake yanatoa hamasa kwa wanawake wanaotamani kuingia kwenye fani ya urubani, yakionyesha kuwa kwa bidii na uvumilivu, hakuna ndoto isiyowezekana. . #womeninaviation #emiratesairline #aviationcareer #aviation #dreamliner #aviatamedia #aviationtanzania"

https://www.instagram.com/p/DGkqZ0DN41Z/?igsh=MXNqeW45aWFqb2M5cA== *Gökçe Kübra, rubani wa kwanza w...

Aviation Tanzania on Instagram: "Miscommunication Leads to Near-Miss Incident at Chicago Midway Airport A serious runway safety incident occurred at Chicago Midway International Airport on Tuesday morning when a private jet crossed an active runway just as a Southwest Airlines flight was about to land. According to air traffic control (ATC) communications, the FlexJet Flight LXJ560 pilot was repeatedly instructed to "hold short" of Runway 31C but did not comply correctly. Instead, the private jet moved onto the live runway, creating a dangerous situation. At that moment, Southwest Airlines Flight WN2504 was descending for landing. To avoid a collision, the Southwest pilot quickly aborted the landing and performed a go-around. Despite repeated instructions, the private jet proceeded across the runway, prompting the Southwest pilot to take evasive action. . #atc #southwestairlines #safety #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"

https://www.instagram.com/reel/DGidNgotM3r/?igsh=MXZlZXFxNnRoNGNiMQ== *Miscommunication Leads to Ne...

Aviation Tanzania on Instagram: "Wanandoa wadai kulazimishwa kukaa pembeni ya mwili wa marehemu kwa masaa manne ndani ya ndege. Wanandoa wawili, Mitchell Ring na Jennifer Colin wamedai kuwa walilazimishwa kukaa kwa masaa manne pembeni ya mwili wa mwanamke aliyefariki kwenye ndege ya Qatar Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka Australia hadi Qatar. Wanandoa hao walikuwa wakitokea Melbourne kuelekea Doha, mji mkuu wa Qatar, wiki iliyopita, masaa kumi baada ya ndege hiyo kuanza safari, mwanamke mmoja alitoka ndani ya choo na kuanguka kisha kupoteza maisha mbele yao. Wawili hao walieleza kwenye kipindi cha habari cha Australia “A Current Affair” siku ya Jumapili kuwa walifanya kila jitihada kuokoa maisha ya mwanamke yule, lakini ilishindikana, jambo ambalo lilikuwa gumu kutazama, alisema Ring. Ring alisema wafanyakazi wa ndege waliuweka mwili wa mwanamke huyo kwenye kiti kilichokuwa wazi karibu nao kwa masaa manne yaliyosalia ya safari yao. Walieleza kuwa,Bi.Jeniffer alikuwa pembeni ya mumewe Ring, wakiwa kwenye mstari wa viti vinne wahudumu walimwambia Jennifer ahamie upande wa pili wa mumewe naye alikubali bila shida, kisha wakauweka mwili wa mwanamke huyo kwenye kiti alichokuwa amekaa Jennifer mwanzoni. Wanandoa hao walisema wafanyakazi wa ndege hawakuwaruhusu kubadilisha viti kwa kipindi chote cha safari na waliwaomba wabaki kwenye viti walivyokuwa hadi wahudumu wa matibabu walipowasili. Qatar Airways, ambayo inamilikiwa na serikali ya Qatar, ilitoa taarifa siku ya Jumatatu ikitoa pole kwa familia ya abiria ambaye alifariki ndani ya ndege yao kwa bahati mbaya. Waliomba msamaha kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika tukio hilo, na walikuwa kwenye mchakato wa kuwasiliana na abiria kulingana na sera na taratibu zao. . Chanzo-NBC News #qatarairways #deathonboard #aviationtanzania✈️ #AviationTanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈ #aviatamedia"

https://www.instagram.com/p/DGiE2VutzUF/?igsh=NmRhc29sdmxlZDB6 *Wanandoa wadai kulazimishwa kukaa p...

Aviation Tanzania on Instagram: "Abiria apaka mafuta ya upako kwenye ndege kabla ya kupanda,kujikinga na ajali. Kufuatia ongezeko la ajali za ndege nchini Marekani, mwanamke mmoja katika mji wa Orlando jimbo la Florida ameonekana akipaka mafuta ya upako kwenye ndege kabla ya kupanda akiamini kuwa ndio kinga dhidi ya ajali. Katika video iliyochapishwa na Desiree Salter, Jumamosi ya Februari 15 ilimuonyesha akifanya tendo hilo huku akisali kabla ya kuingia ndani ya ndege. Kitendo hiki kimeibua mijadala, hasa katika wakati huu ambapo wasiwasi umetawala kwa baadhi ya abiria wakihofia usalama katika safari za anga kufuatia matukio kadhaa ya ajali za ndege nchini Marekani na sehemu nyingine duniani. Ripoti mbalimbali zimeonyesha kuwa ongezeko la ajali limefanya baadhi ya wasafiri kuchukua tahadhari zisizo za kawaida kabla ya kupanda ndege. . #planecrash #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviatamedia #aviationsafety #aviata #aviatamedia"

https://www.instagram.com/reel/DGgTZO8to1t/?igsh=MW4yenp2Z2x6ZmY5Yg== *Abiria apaka mafuta ya upako...