Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 21, 2025 at 05:23 AM
https://www.instagram.com/reel/DJ51XE4sSyW/?igsh=MTl2NGk2azRwMWltZw== *Mandarin Airlines,ATR 72-600 yarudi kwa dharura Kaohsiung baada ya mfuniko wa injini kufunguka ikiwa safarini.* Ndege ya Mandarin Airlines aina ya ATR 72-600 yenye namba ya usajili B-16853 imelazimika kurejea kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kaohsiung, Taiwan, baada ya mfuniko wa ndani wa injini ya kushoto kufumuka ikiwa takribani futi 4,000 juu ya usawa wa bahari. Ndege hiyo ilikuwa ikifanya safari namba AE301 kutoka Kaohsiung kuelekea Kinmen na tatizo hilo lilitokea muda mfupi baada ya kupaa kupitia njia ya kurukia namba 09. Rubani alisitisha mwinuko na kuamua kurejea Kaohsiung, ambapo aliweza kutua salama takriban dakika 15 baada ya kuondoka. Abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walisema kuwa ndege ilianza kutikisika ghafla, na walipoangalia nje waliona kifuniko cha injini kikining’inia na kuyumba kwa nguvu kutokana na upepo, hali iliyowatia hofu kubwa. Hakuna majeruhi waliothibitishwa na mamlaka, na uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha hitilafu hiyo ya kiufundi. #emergencylanding #mandarinairlines #atr72600✈️ #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments