
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 5, 2025 at 07:39 AM
https://www.instagram.com/reel/DKgsrqAtvdi/?igsh=MXQ0ZGxrNjM0ZjZzeA==
*Akamatwa akiendesha Gari Kwenye Eneo Lililozuiliwa, Uwanja wa Ndege wa O’Hare*
Mwanaume mwenye umri wa miaka 36 amekamatwa baada ya kuendesha gari hadi katika eneo lililozuiliwa (Secured areas) la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O’Hare, na kupita katika njia za kurukia na kutua ndege (runways).
Tukio hilo lilitokea Mei 20, 2025, ambapo mwanaume huyo aliripotiwa kuendesha gari kwa umbali wa maili kadhaa ndani ya uwanja huo kabla ya kukamatwa na mamlaka husika.
Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo aliingia katika eneo hilo bila kukusudia pasi na kibali wala mamlaka ya kisheria ya kuwepo hapo.
Huku mamlaka za usalama zikiendelea kukabiliwa na shinikizo la kuzuia watu kuingia kiholela katika njia za kurukia ndege na maeneo ya ndege katika viwanja vikuu vya ndege nchini Marekani, hatua kali zimeanza kuchukuliwa,dhidi ya watu wanaopenya katika maeneo hayo kwa njia za siri kupitia vizuizi au uzio, pamoja na utoaji wa taarifa kuhusu matukio hayo ya ukiukwaji wa usalama.
#airport #truckdrivers #ohareairport #securedareas #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates