Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 10, 2025 at 01:16 PM
https://www.instagram.com/reel/DKuLKHJtsYv/?igsh=M2V0eGw5enRld3E3 *Ndege zakaribia kugongana katika uwanja wa ndege wa Costa Esmeralda.* Ndege ya kifahari aina ya phenom 300 hivi karibuni ilikaribia kugongana angani na helikopta katika uwanja wa ndege wa Esmeralda, ulioko Porto Belo, jimbo la Santa Catarina, Brazil. Tukio hilo lilitokea Juni 8,2025 wakati ndege zote mbili zilipokuwa zinaanza kuruka kutoka ardhini (taking off) kutoka kwenye uwanja huo. Kwa kawaida uwanja huo hauendeshwi na mnara wa kuongoza ndege (air traffic control), jambo linalowalazimu marubani wenyewe kuhakikisha usalama na kugawana maeneo ya kuruka katika anga hilo. Mashuhuda na vyanzo vya ndani vilieleza kuwa kulikuwa na umbali wa kutosha kati ya ndege hizo mbili, ingawa tukio hilo lilikuwa la hatari na lingeweza kusababisha ajali kubwa iwapo mambo yangeenda tofauti. #atc #esmeralda #takingoff✈️ #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments