
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 12, 2025 at 09:28 AM
https://www.instagram.com/p/DKy67lktNC1/?igsh=MWZ2dWUyeTJoYWRpcQ==
*Mashirika ya Ndege 46 na Wajumbe 500 Wakutana Katika Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Zanzibar.*
Zaidi ya mashirika ya ndege 46 na wajumbe 500 kutoka mataifa mbalimbali duniani wamekutana visiwani Zanzibar kushiriki Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Afrika (AviaDev Africa), unaofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.
Mkutano huu umezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni mgeni rasmi wa tukio hilo ukiwakutanisha Wakurugenzi Wakuu wa mashirika ya ndege, viongozi wa viwanja vya ndege, maafisa wa bodi za utalii, na wawakilishi wa serikali kutoka Afrika na kwingineko duniani.
Mkutano huo umetajwa kusaidia ongezeko la safari za moja kwa moja visiwani Zanzibar na maeneo mengine ya Afrika kwa njia ya ushirikiano wa kimkakati kati ya sekta binafsi na serikali, ili kuchochea ukuaji wa utalii na uchumi wa ndani.
Mkutano huo unajumuisha majadiliano ya ana kwa ana baina ya mashirika ya ndege na viwanja vya ndege, mijadala ya kitaalamu kuhusu usafiri wa anga, pamoja na maonyesho ya fursa za uwekezaji.
#aviadev #aviation #aviationprofessionals #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviatamedia