Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #aviationenthusiast

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Mashirika ya Ndege 46 na Wajumbe 500 Wakutana Katika Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Zanzibar. Zaidi ya mashirika ya ndege 46 na wajumbe 500 kutoka mataifa mbalimbali duniani wamekutana visiwani Zanzibar kushiriki Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Afrika (AviaDev Africa), unaofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip. Mkutano huu umezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni mgeni rasmi wa tukio hilo ukiwakutanisha Wakurugenzi Wakuu wa mashirika ya ndege, viongozi wa viwanja vya ndege, maafisa wa bodi za utalii, na wawakilishi wa serikali kutoka Afrika na kwingineko duniani. Mkutano huo umetajwa kusaidia ongezeko la safari za moja kwa moja visiwani Zanzibar na maeneo mengine ya Afrika kwa njia ya ushirikiano wa kimkakati kati ya sekta binafsi na serikali, ili kuchochea ukuaji wa utalii na uchumi wa ndani. Mkutano huo unajumuisha majadiliano ya ana kwa ana baina ya mashirika ya ndege na viwanja vya ndege, mijadala ya kitaalamu kuhusu usafiri wa anga, pamoja na maonyesho ya fursa za uwekezaji. #aviadev #aviation #aviationprofessionals #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviatamedia"

https://www.instagram.com/p/DKy67lktNC1/?igsh=MWZ2dWUyeTJoYWRpcQ== *Mashirika ya Ndege 46 na Wajumb...

Aviation Tanzania on Instagram: "Tazama jinsi ndege za zimamoto zinavyoongeza Maji kwa ajili ya kupambana na moto wa nyika. Kila sekunde ina umuhimu, wakati wa kupambana na moto mkali wa nyika ili kuokoa maisha na makazi ya watu. Katika eneo la Andalucía, ndege mbali mbali hufanya zoezi la kwa kuchota maji kutoka kwenye maziwa na mito (jaw dropping maneuvers) kwa muda mfupi tu. Kwa ustadi wa hali ya juu, ndege hizo hujiandaa kwa haraka na kuelekea kwenye moto wa porini kwa kasi kuendelea na zoezi la kuzima moto. Ndege hizi hugeuka kuwa msaada wa dharura Kwa kuwasili katika maeneo ya moto kwa uharaka na kusaidia kudhibiti majanga kabla hayajaleta madhara makubwa. #jawdroppingmaneuvers #firefighter #wildfires #aviation #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKtoIxSNDh1/?igsh=MTBudnhoYnRueWg0Ng== *Tazama jinsi ndege za zimamo...

Aviation Tanzania on Instagram: "Upepo wa injini za ndege kivutio kwa watalii katika Uwanja wa Princess Juliana. Licha ya hatari zinazohusiana na upepo mkali wa injini za ndege (jet blast), huko St. Maarten katika Uwanja wa Ndege wa Princess Juliana, watalii hujitokeza kwa wingi kushuhudia na kufurahia upepo huo unaotokana na injini za ndege wakati ndege inapojiandaa kuanza safari. Pamoja na kuwepo kwa alama za onyo katika maeneo ya karibu na barabara za kurukia ndege (runways), baadhi ya watalii husimama kwa makusudi nyuma ya ndege ili kupata msisimko wa kihisia (adrenaline) kwa kuhisi kishindo cha upepo huo mkali. Jet blast ni upepo wenye kasi kubwa na joto kali, unaotokana na hewa inayotolewa na injini ya ndege kwa nguvu nyingi. Wakati injini inapofanya kazi, husukuma hewa kwa kasi ya zaidi ya kilomita 800 kwa saa (sawa na maili 500 kwa saa), hali inayoufanya upepo huo kuwa na nguvu ya kipekee na hatari kwa binadamu. #jetblast #engine #tourist #princessjulianaairport #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKsW6WAs0KI/?igsh=ejlrbzJ2YWtvdzgx *Upepo wa injini za ndege kivutio...

Aviation Tanzania on Instagram: "Tom Cruise aweka Rekodi ya dunia kwa kuruka na Parachuti ya moto mara 16. Muigizaji mashuhuri wa filamu ,Tom Cruise, ameweka rekodi mpya ya dunia katika Kitabu cha Guinness baada ya kufanikisha kuruka na parachuti inayowaka moto mara 16, akifanya tukio hilo kwa ajili ya filamu yake mpya ya “Mission: Impossible – The Final Reckoning.” Kwa mujibu wa taarifa kutoka Guinness World Records, Cruise sasa ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa mtu wa kwanza duniani kuruka mara nyingi zaidi na parachuti inayowaka moto. Mhariri Mkuu wa Guinness, Craig Glenday, alieleza kuwa Tom Cruise haonekani tu kama shujaa wa filamu bali anaishi maisha ya ushujaa wa kweli. Aliongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na bidii, umakini mkubwa na uwezo wa Cruise kupitiliza mipaka ya kile ambacho muigizaji anaweza kufanya. Cruise aliruka mara 16 ili kuhakikisha kila tukio linafanikiwa ipasavyo, kabla ya kurekodi picha ya mwisho kwa ajili ya filamu hiyo. Katika video iliyochapishwa na Paramount Pictures, Cruise alionekana akizungumza na waratibu wa mandhari hiyo akifafanua kuwa iwapo parachuti hiyo “ingetwist” wakati ikiwa inawaka moto, angeweza kuanza kuzunguka na kuungua akiwa angani. Pia alieleza kuwa ingawa zoezi hilo lilihitaji ujasiri mkubwa, hakuwa na nia ya kuchukua hatari zisizo za lazima. Akiwa makini lakini mwenye ujasiri, Cruise aliendelea na zoezi hilo kwa kuruka kutoka kwenye helikopta, kufungua parachuti na kuiruhusu ianze kuwaka moto jambo alilolirudia mara 16 kwa mafanikio makubwa. Hiyo ilikuwa sehemu ya maandalizi ya filamu ya “Mission: Impossible – The Final Reckoning,” ambayo ni ya nane katika mfululizo wa filamu hizo maarufu ambazo Cruise ameongoza tangu mwaka 1996. #filmmaking #parachute #missionimpossible #cgi #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKpQCGote7z/?igsh=dGgzZmRmeXN6eHU1 *Tom Cruise aweka Rekodi ya dunia...

Aviation Tanzania on Instagram: "Tazama moja ya matukio ya kusisimua zaidi katika historia ya filamu, ambapo nyota wa filamu ya Mission Impossible anaonekana akiruka kutoka kwenye ndege moja hadi nyingine akiwa angani. Kwa kawaida, waandaaji wa filamu hutumia teknolojia ya kompyuta (CGI) kuonesha uhalisia wa matukio kama haya, lakini katika filamu hii, tukio hilo limetekelezwa kwa uhalisia. Mission: Impossible – The Final Reckoning (2025) ni sehemu ya nane na ya mwisho katika mfululizo wa filamu za Mission: Impossible, iliyoongozwa na Christopher McQuarrie na kumshirikisha nyota huyo, Tom Cruise, kama Ethan Hunt. Filamu hii ilizinduliwa rasmi katika Tamasha la Filamu la Cannes tarehe 14 Mei 2025, na ilianza kuonyeshwa katika sinema duniani kote kuanzia tarehe 23 Mei. #filmmaking #missionimpossible #cgi #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKcxgLJM668/?igsh=OGNvaHZ3a2VqYzJk Tazama moja ya matukio ya kusisim...

Aviation Tanzania on Instagram: "Ujuzi mwingine wa muandaaji wa filamu, Tyler Perry, akirusha ndege yake kwa kutumia rimoti. Mwigizaji na mfanyabiashara mashuhuri kutoka nchini Marekani, Tyler Perry, akionyesha kipaji kingine cha kipekee nje ya filamu, kurusha ndege kubwa zinazodhibitiwa kwa rimoti. Katika eneo lake la kifahari, ametenga kiwanja cha kurushia ndege hizo na eneo maalumu kwaajili ya kuhifadhi kuzifanyia matengenezo ndege hizo (hangar). Miongoni mwa ndege anazomiliki ni C-17 Globemaster, HondaJet, na Pilatus PC-24, zote zikiwa ni ndege kubwa za mfano zenye uwezo mkubwa wa kuongozwa kwa rimoti. Tyler Perry alishirikiana na mbunifu maarufu Ramy RC kutengeneza ndege kubwa aina ya Boeing 777-9X kwa gharama ya takriban dola 97,000. Ndege hiyo ina mwonekano wa ndege halisi na huweza hata kutoa moshi wa matairi wakati wa kutua. Kwa sasa ni rubani aliyeidhinishwa, na huirusha ndege yake binafsi aina ya Cirrus SR22T. #rcplane #tylerperry #tylerperrystudios #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKaH6KcsdyS/?igsh=OHZzdW5zb3ZtdHNi *Ujuzi mwingine wa muandaaji wa f...