Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 18, 2025 at 06:59 AM
https://www.instagram.com/reel/DLCF-7ctTCw/?igsh=Y2hjcmc1YTZiNWE0 *Ndege ya Beechcraft King Air 90 yaanguka juu ya jengo la matengenezo ya ndege na kujeruhi watu wawili.* Ndege aina ya Beechcraft King Air 90 imeanguka juu ya jengo la matengenezo ya ndege (hangar) Butler Avionics, katika Uwanja wa Ndege wa New Century Air Center, uliopo katika jimbo la Kansas, Marekani, na kujeruhi watu wawili waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Ajali hiyo imetokea siku ya jana Juni 17,2025 wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijaribu kutua,na badala ya kutua salama kwenye njia yake, ilitua moja kwa moja juu ya paa la jengo hilo. Waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni rubani na mwanafunzi wa urubani ambao wameripotiwa kutoka Salama ndani ya ndege hiyo wakiwa na majeraha madogo na sasa wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya kilicho karibu. #planecrash #beechcraftkingair #hangar #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments