Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #kenyaairways

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Kenya Airways 787-8 Dreamliner Departs JFK for Nairobi. A @officialkenyaairways 787-8 Dreamliner departed from New York’s John F. Kennedy International Airport (JFK) on its long journey to Nairobi, Kenya, on Thursday. The departure was captured live during Airline Videos Live’s broadcast from the TWA Hotel patio deck, offering viewers a striking view of the aircraft as it took off. #airline #kenyaairways #kq #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKWYg8Rsa-G/?igsh=MXZyYXZjamExcHJ1aA== *Kenya Airways 787-8 Dreamlin...

To our crew that never stops smiling, serving, or ...

To our crew that never stops smiling, serving, or soaring; today, we celebrate you. Happy Internati...

Aviation Tanzania on Instagram: "Kenya Airways yapata Bilioni 4.6 kutokana na tiketi zilizoisha muda bila kutumiwa na abiria. Shirika la ndege la Kenya Airways limeingiza mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kutokana na tiketi ambazo hazikutumika ndani ya kipindi cha miezi 13 tangu ziliponunuliwa na abiria. Taarifa ya shirika hilo imeonesha kuwa mapato yakiyotokana na tiketi zilizopitwa na muda yameongezeka kwa asilimia 9.4 kutoka bilioni 4.2 mwaka uliopita, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka mitano. Kwa kawaida, Kenya Airways huuza tiketi mapema na huzihesabu kama madeni ya muda mfupi kwenye vitabu vyao vya fedha. Tiketi hizo hubadilika na kuwa mapato halali iwapo abiria atasafiri au atashindwa kusafiri ndani ya muda wa mwaka mmoja. Mkuu wa Idara ya Bei na Usimamizi wa Mapato katika shirika hilo, Jackson Kamande, amesema kuwa sera ya matumizi ya tiketi ya shirika hilo inalingana na viwango vya kimataifa, ambapo tiketi huwa halali kwa kipindi cha miezi 12 hadi 13 tangu zinunuliwe. Ongezeko hili la mapato limetokana na ongezeko la safari na uwekaji nafasi za tiketi kutoka kwa wateja wa shirika hilo. Chanzo-NTV Kenya #airlinerevenue #kenyaairways #kq #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKMYnRpMAcq/?igsh=OGhhb2l6emEwaWsx *Kenya Airways yapata Bilioni 4.6 ku...

As the crescent moon graces the sky, we, at #ThePr...

As the crescent moon graces the sky, we, at #ThePrideofAfrica, extend our warmest wishes for a bless...

Aviation Tanzania on Instagram: "Captain Irene Koki Mutungi, mwanamama mwenye historia ya kipekee katika sekta ya anga barani Afrika kwa kuwa ndiye rubani wa kwanza mwanamke barani Afrika kuendesha ndege ya aina ya Boeing 787 Dreamliner. Alizaliwa mwaka 1976 nchini Kenya, ambapo baba yake alikuwa rubani mwenye leseni ya kuendesha ndege za biashara (Commercial Pilot Licence) akifanya kazi na shirika la ndege la Kenya Airways. Koki alisoma katika shule ya Moi Girls iliyopo nchini Nairobi, na baada ya kumaliza elimu ya sekondari mwaka 1992 akiwa na miaka 17, alianza kujifunza urubani. Safari yake ya anga ilianza katika shule ya Wilson Airport nchini Nairobi, ambapo alihitimu na kupata leseni ya kuendesha ndege binafsi (Private Pilot Licence). Aliendelea na mafunzo ya urubani katika mji wa Oklahoma nchini Marekani, ambapo alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege za biashara kutoka Mamlaka ya anga nchini Marekani, FAA. Mwaka 1995, Koki alirejea Kenya na kuajiriwa katika shirika la ndege la Kenya Airways, akiwa mwanamke wa kwanza rubani katika taifa hilo. Alidumu katika rekodi hii kwa miaka sita kabla ya Kenya kupata rubani mwingine mwanamke. Mwaka 2004, Irene alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege kubwa za abiria, na kuwa rubani wa kwanza wa kike Afrika kupata leseni hiyo. Koki alirusha ndege za aina mbalimbali, zikiwemo Boeing 737 hadi Boeing 767. Hatimaye, alikamilisha mafunzo yake na kufuzu kuendesha ndege za Dreamliner, na Aprili 15, 2014, waajiri wake walimtangaza kama mwanamke wa kwanza kuwahi kuendesha Dreamliner barani Afrika. Mwaka 2014, aliandika historia kwa kufuzu kuwa Captain wa ndege hiyo ya kisasa. Captain Irene anajulikana pia kwa mchango wake katika kutoa mwongozo na kuwahamasisha marubani wachanga, hasa wanawake wanaotamani kuingia katika fani hii. Kutokana na mafanikio yake makubwa, Captain Koki amepokea tuzo nyingi za kutambua mchango wake katika sekta ya anga. Umahiri wake ulimfanya atambuliwe na CNN kama mmoja wa viongozi wanaochochea mabadiliko barani Afrika, heshima inayodhihirisha athari chanya ya safari yake ya urubani. @flygirl_koki @officialkenyaairways #womeninaviation #kenyaairways #aviationcareer #aviation #dreamliner #aviatamedia #aviationtanzania"

https://www.instagram.com/p/DGdKJTRNHee/?igsh=MWZmang4MTFlMXR1aQ== *Huyu ndiye, Rubani wa Kwanza mw...

Kenya Airways has signed a landmark MOU with Londo...

Kenya Airways has signed a landmark MOU with London Metropolitan University, paving the way for cutt...

Aviation Tanzania on Instagram: "Kenya Airways yajipanga kuongeza ndege 50 kwa kipindi cha miaka mitano. Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ) limetangaza mpango wa kuongeza zaidi ya ndege 50 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha shirika hilo. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bw.Allan Kilavuka katika mahojiano na Shirika la habari la NTV na kuweka wazi kuwa lengo la shirika hilo ni kuimarisha uwezo wake wa uendeshaji kutoka hadhi ya sasa ya "sub-scale" hadi kiwango endelevu kitakachowezesha usimamizi mzuri wa gharama za uendeshaji. Hata hivyo, juhudi za kutafuta mwekezaji wa kimkakati kwa sasa zimesitishwa ambapo serikali pamoja na wawekezaji wa shirika hilo, wameomba muda zaidi wa kupata mshirika sahihi wa kibiashara. Wakati huu, KQ inazingatia kuongeza uwezo wa kuhudumia abiria kwa kuongeza ndege kupitia ukodishaji wa muda mrefu. Katika hatua nyingine, Kenya Airways imeingia makubaliano ya kukodi ndege kutoka kampuni ya Dubai Aerospace Enterprise (DAE). Mikataba hii ya ukodishaji wa ndege kwa kawaida huchukua kati ya miaka 8 hadi 12, jambo linalowanufaisha pande zote mbili kwa kuwa uwekezaji huo ni wa muda mrefu. Shirika hilo limeeleza kuwa gharama ya kukodisha kila ndege kwa mwezi inakadiriwa kuwa kati ya Dola za Kimarekani 250,000 hadi 400,000. Licha ya mikataba hiyo, Kenya Airways bado inaendelea kufuatilia uwezekano wa kupata mtaji wa ziada ili kuendeleza mkakati wake wa kupanua Shirika hilo huku lengo likiwa ni kuimarisha idadi ya ndege zake na kuboresha nafasi yake katika soko la usafiri wa anga barani Afrika na kimataifa. Chanzo- @ntvkenya . #Airlines #kenyaairways #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviat"

https://www.instagram.com/p/DGU0hMiNbQT/?igsh=MXE4Z2I3YXF4b3l2cA== *Kenya Airways yajipanga kuongez...

Aviation Tanzania on Instagram: "Kenya Airways Yapokea Ndege Mpya, Boeing 737-800. Shirika la ndege la @officialkenyaairways leo Februari,16 2025, limepokea ndege yake mpya aina ya Boeing 737-800, hatua inayoongeza uwezo na urahisi wa mtandao wake wa safari. Ongezeko hili limetajwa kuwa sehemu ya dhamira ya shirika hilo ya kuendelea kutoa huduma bora za usafiri wa anga barani Afrika na nje ya Afrika. . #Airlines #kenyaairways #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviat"

https://www.instagram.com/p/DGP65f8Nan7/?igsh=aTV1djVhMGFnNHA4 *Kenya Airways Yapokea Ndege Mpya, B...

How Kenya Airways Ensures Your Safety in the Skies || #KQImpact

Safety isn’t just a priority, it’s our foundation. From intensive training to real-life emergency si...

Aviation Tanzania on Instagram: "Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nigeria yaituhumu Kenya Airways kwa kuwadhalilisha abiria wa Nigeria. Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Nigeria (NCAA) imechukua hatua kali za kisheria dhidi ya shirika la ndege la Kenya Airways kwa kukiuka mara kwa mara kanuni za ulinzi wa haki za abiria wa Nigeria. Mamlaka hiyo inalituhumu shirika hilo kwa kushindwa kurudisha fedha za fidia kwa abiria waliopoteza mizigo yao, pamoja na kuwadhalilisha abiria. Mgogoro huu umechochewa na tukio lililomhusisha abiria wa Nigeria, Gloria Omisore, ambaye alipewa maelezo yasiyo sahihi kuhusu sifa za kusafiri. Kwa mujibu wa NCAA, Omisore aliwasiliana na Kenya Airways kabla ya safari yake ili kuthibitisha ikiwa anaweza kusafiri kwenye njia fulani bila kuwa na Visa ya Schengen, kwani alikuwa na kibali cha nchini Uingereza. Kenya Airways ilimhakikishia kuwa anaweza kusafiri, lakini baada ya kupanda ndege, alikumbana na vitendo vya uonevu kutoka katika shirika hilo, jambo lililosababisha NCAA kuingilia kati. Akizungumza kuhusu suala hilo, Michael Achimugu, Mkurugenzi wa Masuala ya Umma na Ulinzi wa Watumiaji wa NCAA, alisema kuwa Kenya Airways imekuwa ikiendelea kukiuka kanuni za NCAA mara kwa mara ambapo amebainisha kuwa, awali NCAA ilitoa nafasi kwa shirika hili kurekebisha makosa yake, lakini halikufanya hivyo. Mamlaka hiyo sasa imeweka kitengo chake cha sheria tayari kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya Kenya Airways. Hatahivyo, shirika hilo la ndege limekiri makosa yake katika kisa cha Omisore na kutoa taarifa mpya iliyosahihishwa, likiomba radhi kwa abiria huyo na kwa Mamlaka. Hata hivyo, mbali na tukio hilo, Kenya Airways inakabiliwa na shutuma nyingine, zikiwemo kushindwa kushughulikia malalamiko ya abiria, hususan kurejesha nauli na kushindwa kutoa fidia kwa mizigo iliyopotea. Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa Kenya Airways lazima ihakikishe inazingatia kanuni za ulinzi wa watumiaji au ikabiliwe na adhabu zaidi. Abiria waliokumbwa na matatizo kama haya wanahimizwa kuripoti malalamiko yao kwa NCAA ili kupata suluhisho. . #Airlines #kenyaairways #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviat"

https://www.instagram.com/p/DF7y5yrNPcQ/?igsh=emxpazI1ZHZtNGsx Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nigeria ...