Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 21, 2025 at 06:49 AM
https://www.instagram.com/p/DGU0hMiNbQT/?igsh=MXE4Z2I3YXF4b3l2cA== *Kenya Airways yajipanga kuongeza ndege 50 kwa kipindi cha miaka mitano.* Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ) limetangaza mpango wa kuongeza zaidi ya ndege 50 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha shirika hilo. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bw.Allan Kilavuka katika mahojiano na Shirika la habari la NTV na kuweka wazi kuwa lengo la shirika hilo ni kuimarisha uwezo wake wa uendeshaji kutoka hadhi ya sasa ya "sub-scale" hadi kiwango endelevu kitakachowezesha usimamizi mzuri wa gharama za uendeshaji. Hata hivyo, juhudi za kutafuta mwekezaji wa kimkakati kwa sasa zimesitishwa ambapo serikali pamoja na wawekezaji wa shirika hilo, wameomba muda zaidi wa kupata mshirika sahihi wa kibiashara. Wakati huu, KQ inazingatia kuongeza uwezo wa kuhudumia abiria kwa kuongeza ndege kupitia ukodishaji wa muda mrefu. Katika hatua nyingine, Kenya Airways imeingia makubaliano ya kukodi ndege kutoka kampuni ya Dubai Aerospace Enterprise (DAE). Mikataba hii ya ukodishaji wa ndege kwa kawaida huchukua kati ya miaka 8 hadi 12, jambo linalowanufaisha pande zote mbili kwa kuwa uwekezaji huo ni wa muda mrefu. Shirika hilo limeeleza kuwa gharama ya kukodisha kila ndege kwa mwezi inakadiriwa kuwa kati ya Dola za Kimarekani 250,000 hadi 400,000. Licha ya mikataba hiyo, Kenya Airways bado inaendelea kufuatilia uwezekano wa kupata mtaji wa ziada ili kuendeleza mkakati wake wa kupanua Shirika hilo huku lengo likiwa ni kuimarisha idadi ya ndege zake na kuboresha nafasi yake katika soko la usafiri wa anga barani Afrika na kimataifa. Chanzo- @ntvkenya . #airlines #kenyaairways #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania#aviata #aviat

Comments