
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 11, 2025 at 01:32 PM
https://www.instagram.com/p/DF7y5yrNPcQ/?igsh=emxpazI1ZHZtNGsx
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nigeria yaituhumu Kenya Airways kwa kuwadhalilisha abiria wa Nigeria.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Nigeria (NCAA) imechukua hatua kali za kisheria dhidi ya shirika la ndege la Kenya Airways kwa kukiuka mara kwa mara kanuni za ulinzi wa haki za abiria wa Nigeria.
Mamlaka hiyo inalituhumu shirika hilo kwa kushindwa kurudisha fedha za fidia kwa abiria waliopoteza mizigo yao, pamoja na kuwadhalilisha abiria.
Mgogoro huu umechochewa na tukio lililomhusisha abiria wa Nigeria, Gloria Omisore, ambaye alipewa maelezo yasiyo sahihi kuhusu sifa za kusafiri. Kwa mujibu wa NCAA, Omisore aliwasiliana na Kenya Airways kabla ya safari yake ili kuthibitisha ikiwa anaweza kusafiri kwenye njia fulani bila kuwa na Visa ya Schengen, kwani alikuwa na kibali cha nchini Uingereza. Kenya Airways ilimhakikishia kuwa anaweza kusafiri, lakini baada ya kupanda ndege, alikumbana na vitendo vya uonevu kutoka katika shirika hilo, jambo lililosababisha NCAA kuingilia kati.
Akizungumza kuhusu suala hilo, Michael Achimugu, Mkurugenzi wa Masuala ya Umma na Ulinzi wa Watumiaji wa NCAA, alisema kuwa Kenya Airways imekuwa ikiendelea kukiuka kanuni za NCAA mara kwa mara ambapo amebainisha kuwa, awali NCAA ilitoa nafasi kwa shirika hili kurekebisha makosa yake, lakini halikufanya hivyo.
Mamlaka hiyo sasa imeweka kitengo chake cha sheria tayari kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya Kenya Airways.
Hatahivyo, shirika hilo la ndege limekiri makosa yake katika kisa cha Omisore na kutoa taarifa mpya iliyosahihishwa, likiomba radhi kwa abiria huyo na kwa Mamlaka.
Hata hivyo, mbali na tukio hilo, Kenya Airways inakabiliwa na shutuma nyingine, zikiwemo kushindwa kushughulikia malalamiko ya abiria, hususan kurejesha nauli na kushindwa kutoa fidia kwa mizigo iliyopotea.
Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa Kenya Airways lazima ihakikishe inazingatia kanuni za ulinzi wa watumiaji au ikabiliwe na adhabu zaidi. Abiria waliokumbwa na matatizo kama haya wanahimizwa kuripoti malalamiko yao kwa NCAA ili kupata suluhisho.
.
#airlines #kenyaairways #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviat