
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 21, 2025 at 11:23 AM
https://www.instagram.com/p/DGVT70BtsK_/?igsh=MXFpazk1aWRkMWQzaA==
*Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Shinyanga Wagharimu Bilioni 44.8, kupokea ndege za Bombardier Q400.*
Mradi wa ujenzi wa uwanja wa Ndege, Shinyanga umetajwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 44.8, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga nchini.
Mradi huu unajumuisha ujenzi wa njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 2,200, maingilio ya ndege (Taxiway), maegesho ya ndege (Apron), na jengo la abiria.
Hayo yameelezwa katika ziara ya waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ambaye alibainisha kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka 2023 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoa maelekezo mahsusi ya kuhusu utekelezaji wake.
Prof Mbarawa alifafanua kuwa ingawa mkataba wa mradi huo ulisainiwa mwaka 2017, utekelezaji wake ulikumbwa na changamoto mbalimbali zilizochelewesha kuanza kwake hadi aliporejea katika wizara hiyo mwaka 2022 na kupokea maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Rais kuhusu umuhimu wa kuanza kwa miradi ya viwanja vya ndege vya Shinyanga, Katavi, Kigoma, na Tabora.
Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mradi kutoka Tanroads, Donatus Binemungu, kiwanja hicho kitakuwa na uwezo wa kupokea ndege za ukubwa wa aina ya Bombardier Q400.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, alieleza kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutachangia kukuza uchumi wa mkoa huo, hasa kupitia sekta ya usafirishaji wa madini yanayopatikana katika eneo hilo.
.
#airport #aviationtanzania #shinyanga #shinyangaairport #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata