Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #tanzaniaairportsauthority
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Uwanja wa Ndege wa Arusha Kuanzisha Huduma Saa 24 Kuanzia Desemba. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameeleza kuwa, kuanzia mwezi Desemba 2025, Uwanja wa Ndege wa Arusha utaanza kutoa huduma kwa saa 24 kila siku. RC Makonda ameyasema hayo 17 Juni 2025 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya uboreshaji wa miundombinu katika uwanja huo. Kwa sasa,wakandarasi wanaendelea na zoezi la kuweka taa za kuongozea ndege, hatua muhimu katika maandalizi ya kuufanya uwanja huo kutoa huduma zake Kwa saa 24. Aidha, serikali imepanga kupanua barabara ya kurukia na kutua ndege (runway) hadi kufikia urefu wa mita 500 na Ili kufanikisha hili, serikali inataraajia kuhamisha wakazi wa eneo la Magereza, ambalo lipo karibu na uwanja huo. #airport #tanzaniaairportsauthority #arushaairport #airportinfrastructure #runway #aviationupdate #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzanianews"
https://www.instagram.com/reel/DLAPeI3t18q/?igsh=MXU4NHBqcnA2ZW5zcA== *Uwanja wa Ndege wa Arusha Ku...
Aviation Tanzania on Instagram: "Jaribio la kwanza la kutua Kwa ndege lafanyika katika kiwanja cha ndege cha kimataifa, Msalato. Siku ya Jana Juni 13,2025, ndege aina ya Bombardier Q 400 inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), imetua kwa mafanikio katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya majaribio ya ufanisi wa kiwanja hicho kipya. Hili linakuwa ni jaribio la kwanza la kutua kwa ndege ya kibiashara katika kiwanja hicho ambacho kipo katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kuanza rasmi kwa shughuli za usafiri wa anga. Kukamilika kwa kiwanja cha Ndege cha Msalato kutaiwezesha Tanzania kuwa na jumla ya viwanja vya ndege 62, ambapo vitatu kati yake vitakuwa ni viwanja vya kimataifa. #airport #tanzaniaairportsauthority #msalatointernationalairport #mia #atcl #q400 #aviationupdate #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzanianews"
https://www.instagram.com/reel/DK3wZNyNkpC/?igsh=eXBma3ExaXYwbDhh *Jaribio la kwanza la kutua Kwa n...
Aviation Tanzania on Instagram: "Tazama picha ya Uwanja wa Ndege wa Iringa ulivyokuwa ukionekana katika miaka ya 1960, na namna unavyoonekana kwa sasa. Uwanja huo kwa sasa umeboreshwa kwa 98% na tayari umeanza kupokea ndege za mashirika mbalimbali, zikiwemo ndege za shirika la ndege la Air Tanzania. Maboresho ya uwanja huo yamejumuisha ujenzi wa njia ya kuruka na kutua ndege (Runway) yenye urefu wa mita 2,100 na upana wa mita 30, mnara wa kuongozea ndege, barabara ya maungio (taxiway), maegesho ya ndege, taa za kuongozea ndege, na jengo la muda la abiria.Maboresho hayo kwa ujumla yamegharimu kiasi cha shilingi bilioni 63.74. . #airport #aviationtanzania #iringaairport #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata"
https://www.instagram.com/p/DGlavu7tDE3/?igsh=YmY0MHN3aHluYWpx Tazama picha ya Uwanja wa Ndege wa I...
Aviation Tanzania on Instagram: "Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Kupokea Ndege Kubwa za A380 Baada ya maboresho. Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bertha Bankwa, ameeleza faida mbalimbali zitakazopatikana kufuatia ukarabati wa uwanja huo, ikiwa ni pamoja na kuanza kupokea ndege aina ya A380. Bi. Bertha ameyasema hayo jana, Februari 26, 2025, katika hafla ya utoaji wa fidia kwa wananchi wa eneo la Kipunguni waliopisha zoezi la upanuzi wa kiwanja hicho. Ameeleza kuwa maboresho hayo yanalenga kubadilisha hadhi ya uwanja huo kutoka Daraja la 4C kwenda Daraja la 4F, ambalo ndilo linalokidhi vigezo vya kupokea ndege za aina hiyo. Aidha, maboresho hayo yanatarajiwa kuchangia ongezeko la fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali zinazosaidia shughuli za uendeshaji wa uwanja huo. Miongoni mwa maeneo yatakayonufaika ni hoteli, kumbi, karakana za matengenezo ya ndege, pamoja na maghala ya kuhifadhi mizigo (cargo warehouses). . #airport #aviationtanzania #jnia #juliusnyerereinternationalairport #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata"
https://www.instagram.com/p/DGkjGz0NUpb/?igsh=MWp3Z3BwbGZhcHVjMA== *Uwanja wa Ndege wa Kimataifa w...
Aviation Tanzania on Instagram: "Wananchi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere walipwa fidia ya Bilioni 20. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imelipa fidia ya kiasi cha shilingi bilioni 20 kwa wakazi wa Mtaa wa Kipunguni, Jimbo la Segerea, Dar es Salaam,waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Akizungumza wakati wa hafla ya ulipaji wa fidia, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Abdul Mombokaleo, amesema kuwa malipo hayo ni sehemu ya awamu ya kwanza ya fedha zilizotengwa na serikali kwa ajili ya fidia kwa wananchi waliostahili. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, ni moja kati ya viwanja viwili vikubwa vya kimataifa Tanzania bara, Julai 22, 2024 aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bwana. Mussa Mbura alitangaza ongezeko la abiria wanaowasili katika uwanja wa JNIA kufikia 13% sawa na abiria milioni 3.8 hadi kufikia mwezi Julai 2024, ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo uwanja huo ulipokea jumla ya abiria milioni 2.8. Upanuzi na ukarabati wa uwanja huo, unatarajiwa kuongeza kasi ya matumizi yake na kuboresha zaidi huduma kwa abiria. . #airport #aviationtanzania #jnia #juliusnyerereinternationalairport #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata"
https://www.instagram.com/p/DGi6PFFNGh1/?igsh=a29mbTU5MjZlcjJk *Wananchi waliopisha upanuzi wa uwan...
Aviation Tanzania on Instagram: "Assalaam Air Kushiriki Katika Maonyesho ya Kimataifa ya ITB 2025 nchini Ujerumani. Shirika la ndege nchini Tanzania la @assalaamairtz linatarajia kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya ITB Berlin kwa mwaka 2025. Ushiriki huu unatarajiwa kukuza mtandao wa shirika hilo na kuonyesha huduma maalumu za safari za ndani ya Tanzania pamoja na maeneo bora ya utalii nchini. Maonyesho hayo yatakayofanyika kuanzia Machi 4 hadi 6, 2025 katika mji wa Berlin nchini Ujerumani yatatoa fursa kwa shirika hilo kuungana na wateja wapya na kushiriki maarifa ya tasnia ya usafiri wa anga. Maonyesho ya ITB Berlin ni hafla kubwa zaidi ya biashara katika sekta ya usafiri, ambayo hufanyika kila mwaka, huzileta pamoja kampuni mbalimbali za usafiri, ikitoa fursa ya kipekee ya kujifunza kuhusu mwenendo wa hivi karibuni katika tasnia ya usafiri, kuimarisha uhusiano na mashirika ya kibiashara, na kuwasilisha huduma na bidhaa mpya za mashirika hayo. . #aviation #aviationlovers #avgeek #aircraft #newaircraft #assalaamair #embraer190 #aakia #tcaa #tanzaniaairportsauthority #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"
https://www.instagram.com/p/DGh3wSCtmya/?igsh=cHY0YXZwZ2psNGk1 *Assalaam Air Kushiriki Katika Maony...
Aviation Tanzania on Instagram: "Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato,Clemence Jingu Mbaruku amebainisha chanzo cha ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji wa Dodoma, huku akieleza kuwa uwanja huo ulijengwa baada ya serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka Dar es Salaam kuelekea katika mji wa Dodoma, huku lengo likiwa ni kuboresha uchumi na biashara katika mji huo. Imeelezwa kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutaiweka Tanzania katika nafasi ya kipekee Afrika Mashariki kutokana na mifumo ya kisasa itakayowekwa katika barabara za kurukia na kutua ndege (runways) pamoja na jengo la abiria.Mifumo hii inatarajiwa kurahisisha ufanisi wa safari kwa abiria na kuimarisha ulinzi. Bwana Clemence Jingu Mbaruku ameeleza kuwa Uwanja huu utakuwa na mfumo wa taa za kuongozea ndege wa kisasa (Instrument Landing System - ILS) pamoja na mfumo wa ulinzi wa fensi yenye urefu wa kilomita 18. Runway yake ina upana wa mita 60 na urefu wa kilomita 3.6, ikiwezesha kuhudumia ndege kubwa za kimataifa. Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato ulianza rasmi mwaka 2022 na hadi kufikia Januari 2025, mradi huo ulitajwa kufikia 83.5% kwa upande wa miundombinu na 51% kwa upande wa majengo, huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu. . #airport #aviationtanzania #msalatointernationalairport #mia #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata"
https://www.instagram.com/reel/DGdwhzxNM6G/?igsh=djNwaGJtZHI3MXp5 Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Nde...
Aviation Tanzania on Instagram: "Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Shinyanga Wagharimu Bilioni 44.8, kupokea ndege za Bombardier Q400. Mradi wa ujenzi wa uwanja wa Ndege, Shinyanga umetajwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 44.8, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga nchini. Mradi huu unajumuisha ujenzi wa njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 2,200, maingilio ya ndege (Taxiway), maegesho ya ndege (Apron), na jengo la abiria. Hayo yameelezwa katika ziara ya waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ambaye alibainisha kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka 2023 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoa maelekezo mahsusi ya kuhusu utekelezaji wake. Prof Mbarawa alifafanua kuwa ingawa mkataba wa mradi huo ulisainiwa mwaka 2017, utekelezaji wake ulikumbwa na changamoto mbalimbali zilizochelewesha kuanza kwake hadi aliporejea katika wizara hiyo mwaka 2022 na kupokea maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Rais kuhusu umuhimu wa kuanza kwa miradi ya viwanja vya ndege vya Shinyanga, Katavi, Kigoma, na Tabora. Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mradi kutoka Tanroads, Donatus Binemungu, kiwanja hicho kitakuwa na uwezo wa kupokea ndege za ukubwa wa aina ya Bombardier Q400. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, alieleza kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutachangia kukuza uchumi wa mkoa huo, hasa kupitia sekta ya usafirishaji wa madini yanayopatikana katika eneo hilo. . #airport #aviationtanzania #shinyanga #shinyangaairport #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata"
https://www.instagram.com/p/DGVT70BtsK_/?igsh=MXFpazk1aWRkMWQzaA== *Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Shin...