Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 24, 2025 at 06:12 PM
https://www.instagram.com/reel/DGdwhzxNM6G/?igsh=djNwaGJtZHI3MXp5 Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato,Clemence Jingu Mbaruku amebainisha chanzo cha ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji wa Dodoma, huku akieleza kuwa uwanja huo ulijengwa baada ya serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka Dar es Salaam kuelekea katika mji wa Dodoma, huku lengo likiwa ni kuboresha uchumi na biashara katika mji huo. Imeelezwa kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutaiweka Tanzania katika nafasi ya kipekee Afrika Mashariki kutokana na mifumo ya kisasa itakayowekwa katika barabara za kurukia na kutua ndege (runways) pamoja na jengo la abiria.Mifumo hii inatarajiwa kurahisisha ufanisi wa safari kwa abiria na kuimarisha ulinzi. Bwana Clemence Jingu Mbaruku ameeleza kuwa Uwanja huu utakuwa na mfumo wa taa za kuongozea ndege wa kisasa (Instrument Landing System - ILS) pamoja na mfumo wa ulinzi wa fensi yenye urefu wa kilomita 18. Runway yake ina upana wa mita 60 na urefu wa kilomita 3.6, ikiwezesha kuhudumia ndege kubwa za kimataifa. Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato ulianza rasmi mwaka 2022 na hadi kufikia Januari 2025, mradi huo ulitajwa kufikia 83.5% kwa upande wa miundombinu na 51% kwa upande wa majengo, huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu. . #airport #aviationtanzania #msalatointernationalairport #mia #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata

Comments