
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 25, 2025 at 05:50 PM
https://www.instagram.com/reel/DGgTZO8to1t/?igsh=MW4yenp2Z2x6ZmY5Yg==
*Abiria apaka mafuta ya upako kwenye ndege kabla ya kupanda,kujikinga na ajali.*
Kufuatia ongezeko la ajali za ndege nchini Marekani, mwanamke mmoja katika mji wa Orlando jimbo la Florida ameonekana akipaka mafuta ya upako kwenye ndege kabla ya kupanda akiamini kuwa ndio kinga dhidi ya ajali.
Katika video iliyochapishwa na Desiree Salter, Jumamosi ya Februari 15 ilimuonyesha akifanya tendo hilo huku akisali kabla ya kuingia ndani ya ndege.
Kitendo hiki kimeibua mijadala, hasa katika wakati huu ambapo wasiwasi umetawala kwa baadhi ya abiria wakihofia usalama katika safari za anga kufuatia matukio kadhaa ya ajali za ndege nchini Marekani na sehemu nyingine duniani.
Ripoti mbalimbali zimeonyesha kuwa ongezeko la ajali limefanya baadhi ya wasafiri kuchukua tahadhari zisizo za kawaida kabla ya kupanda ndege.
.
#planecrash #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviatamedia #aviationsafety #aviata #aviatamedia