
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 26, 2025 at 06:10 PM
https://www.instagram.com/p/DGi6PFFNGh1/?igsh=a29mbTU5MjZlcjJk
*Wananchi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere walipwa fidia ya Bilioni 20.*
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imelipa fidia ya kiasi cha shilingi bilioni 20 kwa wakazi wa Mtaa wa Kipunguni, Jimbo la Segerea, Dar es Salaam,waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza wakati wa hafla ya ulipaji wa fidia, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Abdul Mombokaleo, amesema kuwa malipo hayo ni sehemu ya awamu ya kwanza ya fedha zilizotengwa na serikali kwa ajili ya fidia kwa wananchi waliostahili.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, ni moja kati ya viwanja viwili vikubwa vya kimataifa Tanzania bara, Julai 22, 2024 aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bwana. Mussa Mbura alitangaza ongezeko la abiria wanaowasili katika uwanja wa JNIA kufikia 13% sawa na abiria milioni 3.8 hadi kufikia mwezi Julai 2024, ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo uwanja huo ulipokea jumla ya abiria milioni 2.8.
Upanuzi na ukarabati wa uwanja huo, unatarajiwa kuongeza kasi ya matumizi yake na kuboresha zaidi huduma kwa abiria.
.
#airport #aviationtanzania #jnia #juliusnyerereinternationalairport #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata