Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 27, 2025 at 09:23 AM
https://www.instagram.com/p/DGkjGz0NUpb/?igsh=MWp3Z3BwbGZhcHVjMA== *Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Kupokea Ndege Kubwa za A380 Baada ya maboresho.* Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bertha Bankwa, ameeleza faida mbalimbali zitakazopatikana kufuatia ukarabati wa uwanja huo, ikiwa ni pamoja na kuanza kupokea ndege aina ya A380. Bi. Bertha ameyasema hayo jana, Februari 26, 2025, katika hafla ya utoaji wa fidia kwa wananchi wa eneo la Kipunguni waliopisha zoezi la upanuzi wa kiwanja hicho. Ameeleza kuwa maboresho hayo yanalenga kubadilisha hadhi ya uwanja huo kutoka Daraja la 4C kwenda Daraja la 4F, ambalo ndilo linalokidhi vigezo vya kupokea ndege za aina hiyo. Aidha, maboresho hayo yanatarajiwa kuchangia ongezeko la fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali zinazosaidia shughuli za uendeshaji wa uwanja huo. Miongoni mwa maeneo yatakayonufaika ni hoteli, kumbi, karakana za matengenezo ya ndege, pamoja na maghala ya kuhifadhi mizigo (cargo warehouses). . #airport #aviationtanzania #jnia #juliusnyerereinternationalairport #avgeek #tanzaniaairport #tanzaniaairportsauthority #tanzania🇹🇿 #aviationtanzaniaupdates #aviata

Comments