
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 2, 2025 at 06:24 PM
https://www.instagram.com/reel/DKaH6KcsdyS/?igsh=OHZzdW5zb3ZtdHNi
*Ujuzi mwingine wa muandaaji wa filamu, Tyler Perry, akirusha ndege yake kwa kutumia rimoti.*
Mwigizaji na mfanyabiashara mashuhuri kutoka nchini Marekani, Tyler Perry, akionyesha kipaji kingine cha kipekee nje ya filamu, kurusha ndege kubwa zinazodhibitiwa kwa rimoti.
Katika eneo lake la kifahari, ametenga kiwanja cha kurushia ndege hizo na eneo maalumu kwaajili ya kuhifadhi kuzifanyia matengenezo ndege hizo (hangar).
Miongoni mwa ndege anazomiliki ni C-17 Globemaster, HondaJet, na Pilatus PC-24, zote zikiwa ni ndege kubwa za mfano zenye uwezo mkubwa wa kuongozwa kwa rimoti.
Tyler Perry alishirikiana na mbunifu maarufu Ramy RC kutengeneza ndege kubwa aina ya Boeing 777-9X kwa gharama ya takriban dola 97,000. Ndege hiyo ina mwonekano wa ndege halisi na huweza hata kutoa moshi wa matairi wakati wa kutua.
Kwa sasa ni rubani aliyeidhinishwa, na huirusha ndege yake binafsi aina ya Cirrus SR22T.
#rcplane #tylerperry #tylerperrystudios #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates