
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 8, 2025 at 03:21 PM
https://www.instagram.com/reel/DKpQCGote7z/?igsh=dGgzZmRmeXN6eHU1
*Tom Cruise aweka Rekodi ya dunia kwa kuruka na Parachuti ya moto mara 16.*
Muigizaji mashuhuri wa filamu ,Tom Cruise, ameweka rekodi mpya ya dunia katika Kitabu cha Guinness baada ya kufanikisha kuruka na parachuti inayowaka moto mara 16, akifanya tukio hilo kwa ajili ya filamu yake mpya ya “Mission: Impossible – The Final Reckoning.”
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Guinness World Records, Cruise sasa ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa mtu wa kwanza duniani kuruka mara nyingi zaidi na parachuti inayowaka moto. Mhariri Mkuu wa Guinness, Craig Glenday, alieleza kuwa Tom Cruise haonekani tu kama shujaa wa filamu bali anaishi maisha ya ushujaa wa kweli. Aliongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na bidii, umakini mkubwa na uwezo wa Cruise kupitiliza mipaka ya kile ambacho muigizaji anaweza kufanya.
Cruise aliruka mara 16 ili kuhakikisha kila tukio linafanikiwa ipasavyo, kabla ya kurekodi picha ya mwisho kwa ajili ya filamu hiyo. Katika video iliyochapishwa na Paramount Pictures, Cruise alionekana akizungumza na waratibu wa mandhari hiyo akifafanua kuwa iwapo parachuti hiyo “ingetwist” wakati ikiwa inawaka moto, angeweza kuanza kuzunguka na kuungua akiwa angani. Pia alieleza kuwa ingawa zoezi hilo lilihitaji ujasiri mkubwa, hakuwa na nia ya kuchukua hatari zisizo za lazima.
Akiwa makini lakini mwenye ujasiri, Cruise aliendelea na zoezi hilo kwa kuruka kutoka kwenye helikopta, kufungua parachuti na kuiruhusu ianze kuwaka moto jambo alilolirudia mara 16 kwa mafanikio makubwa.
Hiyo ilikuwa sehemu ya maandalizi ya filamu ya “Mission: Impossible – The Final Reckoning,” ambayo ni ya nane katika mfululizo wa filamu hizo maarufu ambazo Cruise ameongoza tangu mwaka 1996.
#filmmaking #parachute #missionimpossible #cgi #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates