Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 9, 2025 at 08:20 PM
https://www.instagram.com/reel/DKsW6WAs0KI/?igsh=ejlrbzJ2YWtvdzgx *Upepo wa injini za ndege kivutio kwa watalii katika Uwanja wa Princess Juliana.* Licha ya hatari zinazohusiana na upepo mkali wa injini za ndege (jet blast), huko St. Maarten katika Uwanja wa Ndege wa Princess Juliana, watalii hujitokeza kwa wingi kushuhudia na kufurahia upepo huo unaotokana na injini za ndege wakati ndege inapojiandaa kuanza safari. Pamoja na kuwepo kwa alama za onyo katika maeneo ya karibu na barabara za kurukia ndege (runways), baadhi ya watalii husimama kwa makusudi nyuma ya ndege ili kupata msisimko wa kihisia (adrenaline) kwa kuhisi kishindo cha upepo huo mkali. Jet blast ni upepo wenye kasi kubwa na joto kali, unaotokana na hewa inayotolewa na injini ya ndege kwa nguvu nyingi. Wakati injini inapofanya kazi, husukuma hewa kwa kasi ya zaidi ya kilomita 800 kwa saa (sawa na maili 500 kwa saa), hali inayoufanya upepo huo kuwa na nguvu ya kipekee na hatari kwa binadamu. #jetblast #engine #tourist #princessjulianaairport #aviationenthusiast #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments