
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 12, 2025 at 01:12 PM
https://www.instagram.com/p/DKzUSkwNDdj/?igsh=MTIwdWdyazllYTlkeQ==
*Polisi Wathibitisha Hakuna Aliyenusurika Katika Ajali ya Ndege ya Air India.*
Polisi nchini India wamethibitisha kuwa hakuna mtu aliyenusurika katika ajali ya ndege ya Air India aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyotokea mchana wa leo, dakika chache baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Ahmedabad kuelekea London.
Kwa mujibu wa mamlaka za usalama, ndege hiyo ilianguka kwenye jengo la bweni la Chuo cha Tiba cha B.J., karibu na uwanja wa ndege, na kusababisha vifo vya wanafunzi kadhaa waliokuwa ndani ya bweni hilo wakati wa ajali.
Maafisa wa polisi wamesema kuwa eneo la tukio tayari limesafishwa kwa asilimia 70 hadi 80, na juhudi za kuwaokoa waliokwama zinaendelea.
Shirika la habari la CNN News-18 limeripoti kuwa, sehemu ya ndege hiyo iliangukia moja kwa moja kwenye eneo la chakula la wanafunzi, likionyesha picha za mabaki ya ndege juu ya paa la jengo na moshi mzito ukifuka angani.
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Uwanja wa Ndege wa Gatwick, kusini mwa London, ikiwa na abiria 230 na wafanyakazi wa ndege 12 (ambao wote wamepoteza maisha). Kwa mujibu wa Air India, abiria hao ni pamoja na raia 169 wa India, 53 Waingereza, 7 kutoka Ureno, na mmoja kutoka Kanada. Watoto 11 na watoto wachanga wawili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Flightradar24, ndege hiyo ilitengenezwa mwaka 2013 na kuanza kuhudumu rasmi katika shirika la Air India mwezi Januari 2014.
Rais wa Uingereza Keir Starmer na Mfalme Charles wote wametuma salamu za rambirambi, huku serikali ya Uingereza ikieleza kuwa inashirikiana kwa karibu na India kufuatilia tukio hilo na kuwasaidia raia wake waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alieleza majonzi yake kupitia ukurasa wake wa X akieleza kuwa ajali hiyo ni ya kuhuzunisha na anaungana kwa pamoja na familia zote zilizoathirika katika kipindi cha maombolezo.
Kampuni ya Boeing imethibitisha kuwa inafuatilia kwa karibu tukio hili na imeanza kushirikiana na mamlaka za India kuchunguza chanzo cha ajali.
Hii ni ajali ya kwanza inayohusisha vifo kwa ndege ya aina ya Dreamliner tangu ianze kutumika mwaka 2011.
#planecrash #airline #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates