Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #boeing787dreamliner

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Ndege ya British Airways, Boeing 787-8 Dreamliner, yapata hitilafu ya kiufundi ikiwa njiani kuelekea India. Ndege ya abiria ya British Airways aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyokuwa ikielekea Chennai, India, siku ya Jana Juni 15,2025 ililazimika kurejea Uwanja wa Ndege wa Heathrow jijini London baada ya kukumbwa na hitilafu ya kiufundi ikiwa angani. Ndege hiyo iliyokuwa ikifanya safari namba BA35, ilipaswa kuondoka Heathrow saa 6:40 mchana lakini ilichelewa na kuondoka saa 7:16 mchana (kwa saa za Uingereza) na Ilitarajiwa kufika Chennai saa 9:30 alfajiri (kwa saa za India). Kwa mujibu wa tovuti ya ufuatiliaji wa safari za ndege, Flightradar24, ndege hiyo ilibaki angani kwa karibu masaa mawili kabla ya kurejea salama Heathrow. Ingawa idadi kamili ya abiria waliokuwemo ndani ya ndege haijajulikana rasmi, video kadhaa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha kuwa ndege hiyo ilikumbwa na tatizo kwenye moja ya sehemu za mabawa (flaps), hali iliyosababisha kurudi kwa dharura. Flightradar24 pia ilionesha kuwa ndege hiyo ilizunguka mara kadhaa angani kabla ya kutua. Katika taarifa iliyotolewa baadaye, British Airways ilithibitisha kuwa ndege hiyo ilitua salama na abiria wote pamoja na wafanyakazi walishuka salama bila matatizo yoyote. Hata hivyo, shirika hilo halikutoa maelezo ya kina kuhusu saa kamili ya kuondoka, muda halisi wa kuwa angani, au idadi ya watu waliokuwemo ndani. Tukio hili limetokea siku chache tu baada ya ajali mbaya ya ndege ya Air India Dreamliner huko Ahmedabad, India, ambapo watu 241 walifariki dunia tukio ambalo limezua taharuki kubwa kuhusu usalama wa ndege aina ya Dreamliner. Chanzo: First post #flightdiversion #boeing787dreamliner #britishairways✈️ #airindia #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DK9MA9rtTap/?igsh=MXRkM2gzeDVsMnl3ZQ== *Ndege ya British Airways, Boein...

Aviation Tanzania on Instagram: "Wote walinusurika Wakiwa Kwenye siti namba 11A: Mwanamuziki wa Thailand na Manusura wa ajali ya Air India. Msanii maarufu wa muziki nchini Thailand, Ruangsak Loychusak, ameibua hisia mpya za majonzi na mshangao baada ya kusimulia kuwa aliwahi kunusurika katika ajali mbaya ya ndege ya Thai Airways mwaka 1998 akiwa amekaa kwenye siti namba 11A – sehemu ileile ambayo Bw.Vishwash Kumar Ramesh, manusura pekee wa ajali ya ndege ya Air India, iliyotokea hivi karibuni, alikuwa ameketi. Ruangsak, ambaye alipata umaarufu mkubwa miaka ya 90 kwa jina la utani “Iron Bones”, alinusurika ajali ya ndege ya Thai Airways TG261 iliyotokea mnamo Disemba 11, 1998, wakati ndege aina ya Airbus ilipoanguka kwenye shamba la mpira huko Surat Thani, na kusababisha vifo vya watu 101. Akiwa ameketi katika kiti namba 11A, alinusurika kwa miujiza lakini aliishi na hofu ya kutumia usafiri wa anga kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi. Ruangsak alipata mshtuko baada ya kusikia kuwa Vishwash Kumar Ramesh, manusura pekee wa ajali ya ndege ya Air India, Boeing 787 Dreamliner iliyotokea tarehe 12 Juni 2025 huko Ahmedabad, India, naye alikuwa ameketi kwenye kiti namba 11A kabla ya ndege hiyo kuanguka katika bweni la chuo kikuu na kuua watu wote waliokuwemo isipokuwa yeye. Kupitia chapisho lake la hisia mitandaoni, Ruangsak alieleza kuwa taarifa hiyo ilimpa msisimko usio wa kawaida na kumfanya atafakari kwa kina namna maisha yalivyojawa na miujiza. Aidha, alitoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa ajali ya Air India, akisema kuwa kiti namba 11A sasa ni zaidi ya namba – ni alama ya matumaini na ushuhuda wa uhai katika mazingira ya maafa. #planecrash #survivor #planecrashsurvivor #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DK6TbhyNW8z/?igsh=MXhxbGh2ZTc5N2ZubA== *Wote walinusurika Wakiwa Kwenye...

Aviation Tanzania on Instagram: "”Blackbox” ya ndege ya Air India yapatikana katika eneo la ajali. Mamlaka za India zimethibitisha kupatikana kwa moja kati ya vifaa viwili vya kurekodi taarifa muhimu (black box) kutoka kwenye ndege ya Air India safari namba AI171, ambayo ilianguka muda mfupi baada ya kuanza kupaa siku ya Jana juni 12,2025. Taarifa kutoka chombo cha habari cha Hindustan Times zinaeleza kuwa kifaa hicho kilipatikana asubuhi ya Leo, ingawa bado haijafahamika kama ni kifaa cha kurekodi mazungumzo ya marubani (Cockpit Voice Recorder) au taarifa za kiufundi za ndege (Flight Data Recorder). Kifaa hicho kinatarajiwa kutoa mwanga kuhusu dakika za mwisho kabla ya ajali hiyo mbaya kutokea. Wachunguzi sasa wameanza kuchambua mabaki ya ndege hiyo aina ya Boeing Dreamliner katika juhudi za kubaini chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vya watu 241 kati ya 242 waliokuwemo, na kuifanya kuwa ajali ya anga mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja. Kwa sasa, chanzo halisi cha ajali hiyo hakijafahamika. Hata hivyo, wataalamu wa usalama wa anga wana matumaini kuwa uchambuzi wa black box hiyo utatoa taarifa muhimu zitakazosaidia kueleza kilichojiri ndani ya dakika chache baada ya ndege hiyo kupaa. Ripoti ya awali ya uchunguzi inatarajiwa kutolewa ndani ya siku chache zijazo. #planecrash #blackbox #planecrashinvestigation #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DK1lkv7taQF/?igsh=M2Q5dWJoZDI1Yzg4 *”Blackbox” ya ndege ya Air India ya...

ॐ शांति... We are deeply saddened by this heartbre...

ॐ शांति... We are deeply saddened by this heartbreaking tragedy. Our thoughts and prayers are with e...

Aviation Tanzania on Instagram: "Polisi Wathibitisha Hakuna Aliyenusurika Katika Ajali ya Ndege ya Air India. Polisi nchini India wamethibitisha kuwa hakuna mtu aliyenusurika katika ajali ya ndege ya Air India aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyotokea mchana wa leo, dakika chache baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Ahmedabad kuelekea London. Kwa mujibu wa mamlaka za usalama, ndege hiyo ilianguka kwenye jengo la bweni la Chuo cha Tiba cha B.J., karibu na uwanja wa ndege, na kusababisha vifo vya wanafunzi kadhaa waliokuwa ndani ya bweni hilo wakati wa ajali. Maafisa wa polisi wamesema kuwa eneo la tukio tayari limesafishwa kwa asilimia 70 hadi 80, na juhudi za kuwaokoa waliokwama zinaendelea. Shirika la habari la CNN News-18 limeripoti kuwa, sehemu ya ndege hiyo iliangukia moja kwa moja kwenye eneo la chakula la wanafunzi, likionyesha picha za mabaki ya ndege juu ya paa la jengo na moshi mzito ukifuka angani. Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Uwanja wa Ndege wa Gatwick, kusini mwa London, ikiwa na abiria 230 na wafanyakazi wa ndege 12 (ambao wote wamepoteza maisha). Kwa mujibu wa Air India, abiria hao ni pamoja na raia 169 wa India, 53 Waingereza, 7 kutoka Ureno, na mmoja kutoka Kanada. Watoto 11 na watoto wachanga wawili. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Flightradar24, ndege hiyo ilitengenezwa mwaka 2013 na kuanza kuhudumu rasmi katika shirika la Air India mwezi Januari 2014. Rais wa Uingereza Keir Starmer na Mfalme Charles wote wametuma salamu za rambirambi, huku serikali ya Uingereza ikieleza kuwa inashirikiana kwa karibu na India kufuatilia tukio hilo na kuwasaidia raia wake waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alieleza majonzi yake kupitia ukurasa wake wa X akieleza kuwa ajali hiyo ni ya kuhuzunisha na anaungana kwa pamoja na familia zote zilizoathirika katika kipindi cha maombolezo. Kampuni ya Boeing imethibitisha kuwa inafuatilia kwa karibu tukio hili na imeanza kushirikiana na mamlaka za India kuchunguza chanzo cha ajali. Hii ni ajali ya kwanza inayohusisha vifo kwa ndege ya aina ya Dreamliner tangu ianze kutumika mwaka 2011. #planecrash #airline #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKzUSkwNDdj/?igsh=MTIwdWdyazllYTlkeQ== *Polisi Wathibitisha Hakuna Aliy...

#Headlines * #Ahmedabad #AirIndia #crash, 242 pe...

#Headlines * #Ahmedabad #AirIndia #crash, 242 people on board * #Plane crashes into #MedicalColle...

Aviation Tanzania on Instagram: "Ndege ya Air India yenye abiria 230+ yapata ajali. Ndege ya Air India aina ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye namba ya usajili (VT-ANB) iliyokuwa ikielekea London Gatwick imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Ahmedabad, nchini India. Ndege hiyo ilikuwa ikifanya safari namba AI171, ikiwa na abiria 230 na wahudumu 12. Kwa sasa zoezi la Uokoaji wa manusura wa ajali hiyo linaendelea likifuatiwa na zoezi uchunguzi. Chanzo: @samchui #planecrash #airline #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKzCX1rN81f/?igsh=MXR0Mjh4a3phcjlkbA== *Ndege ya Air India yenye ab...