Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 13, 2025 at 10:18 AM
https://www.instagram.com/p/DK1lkv7taQF/?igsh=M2Q5dWJoZDI1Yzg4 *”Blackbox” ya ndege ya Air India yapatikana katika eneo la ajali* Mamlaka za India zimethibitisha kupatikana kwa moja kati ya vifaa viwili vya kurekodi taarifa muhimu (black box) kutoka kwenye ndege ya Air India safari namba AI171, ambayo ilianguka muda mfupi baada ya kuanza kupaa siku ya Jana juni 12,2025. Taarifa kutoka chombo cha habari cha Hindustan Times zinaeleza kuwa kifaa hicho kilipatikana asubuhi ya Leo, ingawa bado haijafahamika kama ni kifaa cha kurekodi mazungumzo ya marubani (Cockpit Voice Recorder) au taarifa za kiufundi za ndege (Flight Data Recorder). Kifaa hicho kinatarajiwa kutoa mwanga kuhusu dakika za mwisho kabla ya ajali hiyo mbaya kutokea. Wachunguzi sasa wameanza kuchambua mabaki ya ndege hiyo aina ya Boeing Dreamliner katika juhudi za kubaini chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vya watu 241 kati ya 242 waliokuwemo, na kuifanya kuwa ajali ya anga mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja. Kwa sasa, chanzo halisi cha ajali hiyo hakijafahamika. Hata hivyo, wataalamu wa usalama wa anga wana matumaini kuwa uchambuzi wa black box hiyo utatoa taarifa muhimu zitakazosaidia kueleza kilichojiri ndani ya dakika chache baada ya ndege hiyo kupaa. Ripoti ya awali ya uchunguzi inatarajiwa kutolewa ndani ya siku chache zijazo. #planecrash #blackbox #planecrashinvestigation #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments