Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 16, 2025 at 09:09 AM
https://www.instagram.com/p/DK9MA9rtTap/?igsh=MXRkM2gzeDVsMnl3ZQ== *Ndege ya British Airways, Boeing 787-8 Dreamliner, yapata hitilafu ya kiufundi ikiwa njiani kuelekea India.* Ndege ya abiria ya British Airways aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyokuwa ikielekea Chennai, India, siku ya Jana Juni 15,2025 ililazimika kurejea Uwanja wa Ndege wa Heathrow jijini London baada ya kukumbwa na hitilafu ya kiufundi ikiwa angani. Ndege hiyo iliyokuwa ikifanya safari namba BA35, ilipaswa kuondoka Heathrow saa 6:40 mchana lakini ilichelewa na kuondoka saa 7:16 mchana (kwa saa za Uingereza) na Ilitarajiwa kufika Chennai saa 9:30 alfajiri (kwa saa za India). Kwa mujibu wa tovuti ya ufuatiliaji wa safari za ndege, Flightradar24, ndege hiyo ilibaki angani kwa karibu masaa mawili kabla ya kurejea salama Heathrow. Ingawa idadi kamili ya abiria waliokuwemo ndani ya ndege haijajulikana rasmi, video kadhaa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha kuwa ndege hiyo ilikumbwa na tatizo kwenye moja ya sehemu za mabawa (flaps), hali iliyosababisha kurudi kwa dharura. Flightradar24 pia ilionesha kuwa ndege hiyo ilizunguka mara kadhaa angani kabla ya kutua. Katika taarifa iliyotolewa baadaye, British Airways ilithibitisha kuwa ndege hiyo ilitua salama na abiria wote pamoja na wafanyakazi walishuka salama bila matatizo yoyote. Hata hivyo, shirika hilo halikutoa maelezo ya kina kuhusu saa kamili ya kuondoka, muda halisi wa kuwa angani, au idadi ya watu waliokuwemo ndani. Tukio hili limetokea siku chache tu baada ya ajali mbaya ya ndege ya Air India Dreamliner huko Ahmedabad, India, ambapo watu 241 walifariki dunia tukio ambalo limezua taharuki kubwa kuhusu usalama wa ndege aina ya Dreamliner. Chanzo: First post #flightdiversion #boeing787dreamliner #britishairways✈️ #airindia #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments