Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 17, 2025 at 01:38 PM
https://www.instagram.com/reel/DLAPeI3t18q/?igsh=MXU4NHBqcnA2ZW5zcA== *Uwanja wa Ndege wa Arusha Kuanzisha Huduma Saa 24 Kuanzia Desemba.* Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameeleza kuwa, kuanzia mwezi Desemba 2025, Uwanja wa Ndege wa Arusha utaanza kutoa huduma kwa saa 24 kila siku. RC Makonda ameyasema hayo 17 Juni 2025 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya uboreshaji wa miundombinu katika uwanja huo. Kwa sasa,wakandarasi wanaendelea na zoezi la kuweka taa za kuongozea ndege, hatua muhimu katika maandalizi ya kuufanya uwanja huo kutoa huduma zake Kwa saa 24. Aidha, serikali imepanga kupanua barabara ya kurukia na kutua ndege (runway) hadi kufikia urefu wa mita 500 na Ili kufanikisha hili, serikali inataraajia kuhamisha wakazi wa eneo la Magereza, ambalo lipo karibu na uwanja huo. #airport #tanzaniaairportsauthority #arushaairport #airportinfrastructure #runway #aviationupdate #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzanianews

Comments