
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 20, 2025 at 06:12 AM
https://www.instagram.com/p/DGSLowft_J8/?igsh=aWFleGZzZzBwMnht
*Nchi 10 zinazo miliki ndege zenye umri mrefu zaidi barani Afrika*
Unapopanda ndani ya ndege, huenda ikawa si rahisi kuwaza kuhusu umri wa ndege hiyo na muda ambao ndege hiyo imekuwa ikifanya safari zake, Lakini nyuma ya kila safari nzuri ya ndege, kuna hadithi yake.
Umri wa ndege, unaopimwa tangu safari yake ya kwanza, huonyesha wastani wa miaka ambayo ndege imekuwa ikihudumu katika kundi la ndege za shirika husika.
Kipimo hiki ni kiashiria muhimu kwa mashirika ya ndege na wasafiri, kikionyesha uwiano kati ya uboreshaji wa ndege, gharama za matengenezo, ufanisi wa mafuta, na hali ya abiria kwa ujumla.
Duniani kote, wastani wa umri wa ndege za kibiashara hutofautiana sana. Baadhi ya nchi zina mashirika ya ndege yanayoendeshwa na ndege mpya kabisa, huku mashirika mengine yakiendelea kutumia ndege zenye miundo ya zamani.
Ingawa ndege hizi za zamani zinaweza kukosa baadhi ya huduma zenye kustarehesha na ufanisi wa teknolojia mpya, bado zinatunzwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya usalama.
Barani Afrika, mashirika mengi ya ndege hutumia baadhi ya ndege zenye umri mkubwa zaidi duniani. Hali hii inatokana na changamoto za kifedha, upatikanaji mdogo wa mtaji, na utegemezi wa ndege za zamani zilizonunuliwa kwa mara ya pili.
Kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Planespotter, ndege za nchi ya Somalia zina wastani wa umri wa juu zaidi barani Afrika,huku wastani wake ukifukia miaka 33.9 inafuatiwa na nchi ya Sudan Kusini kwa wastani wa miaka 33, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiwa na ndege zenye wastani wa miaka 30.7.
Chanzo- Business Insider
#airlines #sudanairways #somaliairlines #congoairways #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviat