
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 20, 2025 at 12:58 PM
https://www.instagram.com/reel/DGS58Izt1Uy/?igsh=amVzaWJrMWpkbXQ5
*Ndege mbili zagongana angani, Abiria wa ndege moja wapoteza maisha, ndege nyingine wabaki salama.*
Watu wawili wamepoteza maisha baada ya ndege mbili kugongana angani karibu na Uwanja wa Ndege wa Marana, Arizona, Februari 19,2025.
Ajali hiyo ilihusisha ndege aina ya Cessna 1725 (N463ER) na Lancair 360 MK II (N3602M),ambazo ziligongana karibu na mwisho wa barabara ya ndege namba 12 huku kila moja ikiwa na abiria wawili ndani yake.
Kufuatia ajali hiyo, Lancair ilianguka na kushika moto, na kusababisha vifo vya abiria wake wote wawili na ndege ya Cessna 1725 ilifanikiwa kutua salama, na abiria wote wawili wameripotiwa kuwa salama bila ya majeraha.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Marekani (FAA) na Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri (NTSB) zinafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
.
#accident #planecrash #cessna1725 #lancair #360mk #safety #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv