
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 28, 2025 at 06:50 AM
https://www.instagram.com/p/DGm2UjptyLi/?igsh=dnNubmc2Y3M4N3U0
*Dubai yajenga uwanja wa ndege mkubwa zaidi duniani, utakaohudumia abiria milioni 260.*
Dubai inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa zaidi duniani,unaojulikana kama uwanja wa ndege wa kimataifa wa Al Maktoum, ikiwa imewekeza kiasi cha dola za kimarekani bilioni 35.
Mradi huu wa kisasa uliodhinishwa Aprili 2024 na mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid al-Maktoum,unajumuisha ujenzi wa jengo jipya la abiria, ambalo pia linajulikana kama Dubai World Central, sambamba na ujenzi wa njia tano za ndege (runways), kila moja ikiwa na urefu wa kilomita 4.5, ili kuruhusu ndege kuruka na kutua kwa wakati mmoja.
Vilevile ujenzi wa njia zinazoelekea katika eneo la kupaki magari ambazo zitasaidia kupunguza msongamano na kuboresha muda wa mzunguko wa ndege. Aidha, vituo viwili vya uongozaji wa ndege (Air Traffic control) vitajengwa katika teknolojia ya kisasa, ili kuhakikisha usalama na ufanisi wa shughuli za anga.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Al Maktoum utakapo kamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 260 kila mwaka, ambayo ni mara tano zaidi kuliko uwezo wa sasa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai (DXB).
Vilevile, utakapomalizika uwanja huo, Shughuli zote za ndege kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai (DXB) zitahamia kwenye Uwanja huo ifikapo mwaka 2035.
Mradi huu unalenga kudumisha nafasi ya mji wa Dubai kama kitovu cha kimataifa cha usafiri wa anga na kuweka mazingira bora kwa shughuli za anga za siku zijazo.
.
#dxb #dubai #almakhtoumairport #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata