Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #tcaa
Posts
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewata...
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka Wasafiri wa Ndege ndani na nje ya Nchi kutositi...
Tanzania Nears Completion of Nationwide VHF Communication Upgrade
En 🇬🇧 *#GOOD_TO_KNOW | Tanzania Nears Completion of Nationwide VHF Communication Upgrade* ...
Aviation Tanzania on Instagram: "TCAA na Idara ya uhamiaji wasaini mpango wa kubadilishana taarifa Kidijitali. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania @officialtcaa na Idara ya Uhamiaji @uhamiajitz leo Mei 27,2025 wameingia katika makubaliano rasmi ya kushirikiana katika kubadilishana taarifa kwa njia ya kidijitali, hatua inayolenga kuimarisha usalama wa anga, kuongeza ufanisi wa huduma, na kuboresha takwimu muhimu, hususan katika sekta ya utalii. Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dodoma katika makao makuu ya Idara ya Uhamiaji na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka taasisi zote mbili,yakisiniwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Bi. Anna Makakala. Bw. Msangi alisema kuwa mpango huu umeanzishwa katika kipindi mwafaka ambapo matumizi ya teknolojia ya kisasa yazidi kuongezeka Kwa kasi duniani. If Alieleza kuwa kupitia ushirikiano huo, TCAA itaongeza ufanisi wa operesheni zake, kuimarisha usalama wa anga na kusaidia katika udhibiti bora wa wageni wanaoingia na kutoka nchini kupitia viwanja vya ndege. Kwa upande wake, Kamishna Jenerali Makakala alibainisha kuwa Idara ya Uhamiaji itaendeleza ushirikiano wa karibu na TCAA ili kuhakikisha kuwa taarifa za abiria na safari za anga zinawasilishwa kwa usahihi na kwa wakati. Mpango huu pia unatarajiwa kuboresha ukusanyaji wa takwimu za wageni wanaoingia nchini, jambo litakalosaidia katika kupanga mikakati madhubuti ya kukuza sekta ya utalii na uchumi wa taifa kwa ujumla. #tcaa #tanzaniacivilaviationauthority #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdate"
https://www.instagram.com/p/DKKWl8mMhJF/?igsh=emt0NGtlZG1oMTZi *TCAA na Idara ya uhamiaji wasaini m...
Big moves in aviation! ATCL, TAA, TCAA na TMA sign...
Big moves in aviation! ATCL, TAA, TCAA na TMA sign one game-changing MoU – future of Tanzania’s skie...
Tanzanie : Un système commun de facturation unit désormais les acteurs du secteur aérien
En 🇬🇧 *#GOOD_TO_KNOW | Tanzania’s Aviation Sector Unites with Integrated Payment System Agreeme...
Aviation Tanzania on Instagram: "chuo cha CATC chatunukiwa tuzo kwa Ubora Katika Mafunzo ya Usalama wa Anga. Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kimetunukiwa tuzo ya kimataifa kutokana na ubora wake katika utoaji wa mafunzo ya usalama wa anga kwa mwaka 2024, hatua inayoimarisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya usafiri wa anga barani Afrika. Katika tathmini iliyofanywa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), CATC imeorodheshwa miongoni mwa taasisi tatu bora katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAF), na imeingia kwenye orodha ya taasisi tisa bora za mafunzo ya anga barani Afrika kwa ujumla. Tuzo hiyo iliwasilishwa rasmi tarehe 19 Mei 2025 katika hafla maalum iliyofanyika makao makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya anga akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, alimkabidhi tuzo hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, Dkt. Hamis Mwinyimvua, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa chuo cha CATC katika kukuza usalama wa anga kupitia mafunzo bora na yenye viwango vya kimataifa. #catc #aviationtraining #aviationlovers #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdate"
https://www.instagram.com/p/DJ3ykGPsn2N/?igsh=MWhhb2syamUxMXp5dg== *Chuo cha CATC chatunukiwa tuzo ...
Ndegenyuki (Drone) ni ndege isiyo na rubani inayoo...
Ndegenyuki (Drone) ni ndege isiyo na rubani inayoongozwa na mtu au ngamizi kutoka eneo la mbali na z...
Aviation Tanzania on Instagram: "Assalaam Air Kushiriki Katika Maonyesho ya Kimataifa ya ITB 2025 nchini Ujerumani. Shirika la ndege nchini Tanzania la @assalaamairtz linatarajia kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya ITB Berlin kwa mwaka 2025. Ushiriki huu unatarajiwa kukuza mtandao wa shirika hilo na kuonyesha huduma maalumu za safari za ndani ya Tanzania pamoja na maeneo bora ya utalii nchini. Maonyesho hayo yatakayofanyika kuanzia Machi 4 hadi 6, 2025 katika mji wa Berlin nchini Ujerumani yatatoa fursa kwa shirika hilo kuungana na wateja wapya na kushiriki maarifa ya tasnia ya usafiri wa anga. Maonyesho ya ITB Berlin ni hafla kubwa zaidi ya biashara katika sekta ya usafiri, ambayo hufanyika kila mwaka, huzileta pamoja kampuni mbalimbali za usafiri, ikitoa fursa ya kipekee ya kujifunza kuhusu mwenendo wa hivi karibuni katika tasnia ya usafiri, kuimarisha uhusiano na mashirika ya kibiashara, na kuwasilisha huduma na bidhaa mpya za mashirika hayo. . #aviation #aviationlovers #avgeek #aircraft #newaircraft #assalaamair #embraer190 #aakia #tcaa #tanzaniaairportsauthority #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"
https://www.instagram.com/p/DGh3wSCtmya/?igsh=cHY0YXZwZ2psNGk1 *Assalaam Air Kushiriki Katika Maony...
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanz...
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wa...
Aviation Tanzania on Instagram: "Katika mahojiano na katibu wa Mfuko wa Mafunzo chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bi. Massa Mubuli, ameeleza gharama zilizotumika katika ufadhili wa masomo ya urubani na uhandisi wa ndege kwa kila mnufaika, ambapo imeelezwa kuwa, kila rubani aligharamiwa shilingi milioni 200 za Kitanzania hadi kukamilisha masomo, na kwa upande wa wahandisi kila mmoja aligharamiwa Shilingi milioni 70. Fuatilia mahojiano kamili kupitia chaneli yetu ya YouTube @aviationtanzania. Bonyeza link kwenye bio yetu. . #aviationcareer #tcaatrainingfund #scholarship #aviation #aviationsafety #aviatamedia #aviationtanzaniaupdates #AviationTanzania✈"
https://www.instagram.com/reel/DGOck6YNI-q/?igsh=MW1ocnE4dnFveW95MA== Katika mahojiano na katibu wa...
Aviation Tanzania on Instagram: "TCAA yasisitiza udhibiti wa matumizi ya "drones" kwa usalama wa anga Tanzania. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa onyo kali kwa watumiaji wa ndege zisizo na rubani (drones), ikisisitiza kuwa matumizi yasiyo na vibali yanaweza kuhatarisha usalama wa anga. Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw.Salim Msangi, amebainisha kuwa kumekuwepo na ongezeko la matumizi holela ya drones,kwa watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, hali inayokiuka sheria na kutishia usalama kwa safari za anga. Bwana Msangi amezungumza hayo,leo Februari 17, 2025, katika hafla ya kukabidhi misaada kwa wafungwa wa Gereza Kuu la Karanga, Moshi na kuongeza kuwa sheria inawataka watumiaji wa drones kupata vibali maalum kabla ya kuzitumia. Ameeleza kuwa drones zinapaswa kusajiliwa kama ilivyo kwa ndege nyingine, na matumizi yake lazima yaidhinishwe na mamlaka husika. Msangi amesisitiza kuwa maeneo nyeti kama magereza na taasisi za kijeshi ni marufuku kurusha ndege za drones, na yeyote atakayekiuka sheria atachukuliwa hatua kali, ikiwemo kushtakiwa. Pia, ameonya kuwa matumizi yasiyodhibitiwa yanaweza kusababisha ajali za anga, akitoa tahadhari dhidi ya uwezekano wa drones kugongana na ndege kubwa zinazobeba abiria. . #Airlines #tcaa #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"
https://www.instagram.com/p/DGLvaWRNkaQ/?igsh=cHd4YW5xYWNhYTcx *TCAA yasisitiza udhibiti wa matumi...
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa ...
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa wasiwasi juu ya matumizi mabaya ya ndege zisizo na...