Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #routeexpansion

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Mmoja wa abiria waliosafiri Kwa Mara ya kwanza kutoka Nairobi hadi Arusha (WIL–ARK),Kwa kutumia ndege za shirika la @flightlinktz ameielezea safari hiyo kuwa ya haraka na yenye urahisi mkubwa. #Airlines #flightlink #newroute #routeexpansion #airlinepassenger #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DK_33PYtyzw/?igsh=cGpwY3lrY2lmdGU3 Mmoja wa abiria waliosafiri Kwa M...

Aviation Tanzania on Instagram: "RC Makonda Ashuhudia Safari Mpya ya Flightlink Kutoka Nairobi Hadi Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, @baba_keagan , leo Juni 17,2025 ametembelea katika Uwanja wa Ndege wa Arusha na kushuhudia kwa mara ya kwanza safari mpya ya ndege ya shirika la Flightlink iliyoanzia Uwanja wa Ndege wa Wilson, jijini Nairobi, Kenya hadi uwanja wa ndege wa Arusha. RC Makonda alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Uendeshaji wa Flightlink Bw.Jameel Kassam kuhusu umuhimu wa safari hizo kwa mkoa wa Arusha na maendeleo ya sekta ya utalii na biashara. Safari hii mpya ya moja kwa moja kati ya Arusha (ARK) na Nairobi (WIL) ni ya kwanza kuanzishwa nchini Tanzania, safari ambayo hutumia muda wa Dakika 45. #Airlines #flightlink #newroute #routeexpansion #atr72 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DK9QCgltxDb/?igsh=NjlkaTJnc3dzN3dk *RC Makonda Ashuhudia Safari Mpya ya...

https://www.instagram.com/p/DK7j_6TNByQ/?igsh=MTlq...

https://www.instagram.com/p/DK7j_6TNByQ/?igsh=MTlqM21mcGV4M2M4ag== *Flightlink yazindua safari mpya...

Aviation Tanzania on Instagram: "Katika Mkutano wa Kimaendeleo ya sekta ya anga,Aviadev ,Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la ndege la @airtanzania_atcl Mhandisi Peter Ulanga ameeleza mipango ya hivi karibuni ya shirika hilo ikiwemo kuanzisha safari katika visiwa vya Pemba. #airline #airtanzania #routeexpansion #newaircraft #airtanzania_atcl #aviation #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"

https://www.instagram.com/reel/DKzuwGFNhbb/?igsh=MXFpNmgydWtyMXJnaA== Katika Mkutano wa Kimaendeleo...

Aviation Tanzania on Instagram: "Katika maonyesho ya @kilifair 2025, Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la @flightlinktz , @munawerdhirani ameeleza namna shirika hilo lilivyojipanga kuongeza safari za ndani na nje ya nchi. Safari hizo ni pamoja na zile kati ya Uwanja wa Ndege wa Arusha na uwanja wa ndege wa Wilson zitakazozinduliwa tarehe 15 Juni 2025, pamoja na safari kati ya Zanzibar na Jomo Kenyatta zitakazoanza tarehe 1 Julai 2025. Aidha, Flightlink imepanga kuanzisha safari kati ya Mwanza na Kilimanjaro, zitakazozinduliwa ndani ya mwezi Julai. #Airlines #routeexpansion #flightlink #aviationlovers #aviationcareer #atr72500 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKoSH0Pt-2f/?igsh=MTd5YnNsd204dnNyZw== *Flightlink yapanga kuanzisha...

Aviation Tanzania on Instagram: "Flightlink yashiriki katika maonyesho ya Karibu Kilifair Arusha. Shirika la ndege la @flightlinktz , limeshiriki katika maonyesho ya kibiashara na Utalii ya Karibu Kilifair Kwa mwaka 2025. Maonyesho hayo yaliyozinduliwa siku ya Jana Juni 6,2025 yalihudhuriwa na mgeni rasmi, Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh.Dotto Biteko, yanafanyika katika viwanja vya Magereza jijini Arusha na yanatarajia kuhitimishwa siku ya kesho Juni 08,2025. Zaidi ya makampuni 500 kutoka Afrika mashariki yamepata fursa ya kuonyesha bidhaa na huduma zao katika maonyesho hayo Kwa mwaka huu, maonyesho ambayo yanatazamiwa kukuza zaidi sekta ya utalii wa ndani na nje ya nchi. Flightlink imepata fursa ya kuonyesha na kutangaza zaidi huduma ya safari zake ikiwemo safari mpya zinazotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni zikiwemo safari za ndani na nje ya nchi. Endelea kutufuatilia Kwa habari mbalimbali kuhusu maonyesho ya Karibu Kilifair 2025. #exhibition #airline #flightlink #newroutes #routeexpansion #ys #kilifair2025 #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"

https://www.instagram.com/p/DKm9B4wNwpQ/?igsh=MWhubHIxdXJnM2M3NQ== *Flightlink yashiriki katika mao...

Aviation Tanzania on Instagram: "United Airlines Yaanzisha Safari Yake ya Sita Afrika: Washington–Dakar. Shirika la ndege la @united limeanzisha safari mpya ya moja kwa moja kutoka Washington, D.C. kwenda Dakar, Senegal. Hii ni safari ya sita barani Afrika huku safari nyingine tayari zinafanyika kutoka Washington hadi miji ya Cape Town na Johannesburg nchini Afrika Kusini, Accra nchini Ghana, Lagos nchini Nigeria, na Marrakesh nchini Morocco. Safari ya kwanza ya kuelekea Dakar, ilikuwa na jumla abiria 505, jambo linaloonesha uhitaji mkubwa wa huduma hii ya usafiri wa anga katika miji hiyo. #routeexpansion #airline #unitedairlines #africanflights #dakar #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviatamedia"

https://www.instagram.com/reel/DKUlglSsXFh/?igsh=aXpvZGwzemZ2NzF4 *United Airlines Yaanzisha Safari...

Aviation Tanzania on Instagram: "Air France yarejesha safari za moja kwa moja Kati ya Zanzibar na Ufaransa. Shirika la Ndege la Air France limeanza tena safari za moja kwa moja kati ya Ufaransa na Zanzibar, kufuatia kuwasili kwa ndege yake aina ya Boeing 787-8 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA). Ndege hiyo iliwasili siku ya jumatatu Mei 26, 2025 majira ya saa 2:57 usiku ikiwa na jumla ya abiria 125. Hii ni safari ya kwanza ya moja kwa moja kufanyika tangu mwezi Machi 2025, wakati shirika hilo lilipositisha kwa muda huduma hizo kutokana na msimu mdogo wa abiria (low season). Kwa mujibu wa ratiba mpya, Air France itakuwa ikifanya safari zake za moja kwa moja mara tatu kwa wiki yaani siku za Jumatano, Alhamisi na Jumamosi huku ikifungua fursa zaidi kwa watalii kutoka Ufaransa na mataifa jirani kutembelea visiwa vya Zanzibar. @zaazanzibar #routeexpansion #airline #airfrance #abeidamanikarumeinternationalairport #zanzibarairportauthority #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKKhjs7MIdP/?igsh=MTR3YjhhMmU0eGw0ZA== *Air France yarejesha safari za ...

Aviation Tanzania on Instagram: "Air Tanzania yajipanga kuanza safari za ndani na nje ya nchi Katika maeneo haya. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la @airtanzania_atcl , Mhandisi Peter Ulanga, ametaja maeneo kadhaa ndani na nje ya nchi yanayohitaji kwa kiwango kikubwa huduma ya usafiri wa anga, akieleza kuwa tayari imeanza kuweka mipango kwa ajili ya kufanikisha huduma hizo. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la TBC, Mhandisi Ulanga alisema kuwa ndani ya nchi, maeneo ya Musoma, Shinyanga na hasa Bukoba yanaonesha uhitaji mkubwa wa huduma za ndege na kubainisha kuwa Bukoba ndiyo eneo lenye mahitaji ya juu zaidi, huku serikali ikiwa tayari imewekeza katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo hayo. Kwa upande wa safari za kimataifa, Mhandisi Ulanga alieleza kuwa taifa jirani la Msumbiji limeomba Air Tanzania kuanzisha safari zake kuelekea miji ya Maputo, Beira, Nampula na Pemba. Aidha, shirika hilo pia linaangazia uwezekano wa kuanzisha safari kuelekea visiwa vya Mayotte na Shelisheli, maeneo maarufu kwa vivutio vya utalii na biashara. Katika mipango yake ya ndani zaidi, Air Tanzania inatarajia kufungua safari za moja kwa moja kuelekea visiwa vya Pemba, Mafia na hifadhi ya Serengeti, hasa wakati wa msimu wa utalii, hatua ambayo inalenga kuimarisha utalii wa ndani na kuongeza mapato kwa taifa. Hadi sasa, Shirika la Ndege la ATCL linahudumia maeneo 14 ndani ya nchi. Katika bara la Afrika, linatoa huduma katika vituo 10, na nje ya Afrika linafika katika vituo vitatu. #routeexpansion #airline #airtanzania #airtanzania_atcl #aviationcareer #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DJ_P3Qas5B2/?igsh=ZDNzY2o3cnBqb3Z4 *Air Tanzania yajipanga kuanza sa...

Aviation Tanzania on Instagram: "Kuelekea uzinduzi wa Safari za Arusha–Nairobi, Flightlink yatambuliwa rasmi na na KATA. Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Kampuni ya ndege ya @flightlinktz kuzindua rasmi safari kati ya miji ya Arusha-Nairobi,kampuni hiyo imepokea rasmi Cheti na Uanachama kutoka Chama cha Wakala wa Usafiri wa Ndege Kenya (KATA). Hii ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo katika kuhakiki huduma bora na za kuaminika kwa wateja wake. Kupitia uanachama huu, Flightlink sasa inatambuliwa rasmi kama mshirika wa KATA chama cha kitaaluma kinachowakilisha na kusimamia maslahi ya mawakala wa usafiri nchini Kenya. Flightlink inatarajia kuzindua safari za anga kati ya mji wa Arusha na Nairobi kuanzia mwezi juni 15,2025 ,Safari ambazo zinalenga kurahisisha usafiri kwa wasafiri wa kibiashara, watalii, na wale wanaosafiri kwa shughuli binafsi. #airline #flightlink #kata #routeexpansion #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DJ9D3MhsIiH/?igsh=aDhudnA2eGw3M2Zu *Kuelekea uzinduzi wa Safari za Arus...