Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #aviationlovers

Posts

https://www.instagram.com/p/DK7j_6TNByQ/?igsh=MTlq...

https://www.instagram.com/p/DK7j_6TNByQ/?igsh=MTlqM21mcGV4M2M4ag== *Flightlink yazindua safari mpya...

Aviation Tanzania on Instagram: "Precision Air yatembelea Kituo cha watoto Cornel Ngaleku, kumuenzi muanzilishi wa Shirika hilo. Shirika la ndege la @precisionairtz limepata fursa ya kutembelea Kituo cha Watoto cha Cornel Ngaleku na kutoa msaada wao wa upendo kwa watoto waliopo kituoni hapo. Kupitia ujumbe wake rasmi, shirika hilo limeeleza kuwa, ziara hiyo pia imefanyika Kama namna ya kumuenzi mwanzilishi wa shirika hilo, marehemu Michael Shirima, ambaye ndoto na maono yake bado yanaendelea kuwa dira ya huduma na mshikamano wa kijamii. Kupitia tukio hilo, Precision Air imeeleza kuguswa na furaha iliyosambaa kwenye nyuso za watoto hao, jambo linalothibitisha nguvu ya huruma na mshikamano wa jamii. #Airlines #pw #precisionair #youarewhywefly #aviationlovers #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DK2aM52tiI9/?igsh=MncyMDFtYjBhMzd1 *Precision Air yatembelea Kituo cha ...

Aviation Tanzania on Instagram: "Katika maonyesho ya @kilifair 2025, Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la @flightlinktz , @munawerdhirani ameeleza namna shirika hilo lilivyojipanga kuongeza safari za ndani na nje ya nchi. Safari hizo ni pamoja na zile kati ya Uwanja wa Ndege wa Arusha na uwanja wa ndege wa Wilson zitakazozinduliwa tarehe 15 Juni 2025, pamoja na safari kati ya Zanzibar na Jomo Kenyatta zitakazoanza tarehe 1 Julai 2025. Aidha, Flightlink imepanga kuanzisha safari kati ya Mwanza na Kilimanjaro, zitakazozinduliwa ndani ya mwezi Julai. #Airlines #routeexpansion #flightlink #aviationlovers #aviationcareer #atr72500 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKoSH0Pt-2f/?igsh=MTd5YnNsd204dnNyZw== *Flightlink yapanga kuanzisha...

Aviation Tanzania on Instagram: "TAA yatangaza kuanza Kwa safari mpya za shirika la ndege la Flightlink. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania @tanzaniairports imetangaza kuanza kwa safari mpya za anga za shirika la ndege la @flightlinktz kati ya miji ya Arusha na Nairobi, kuanzia tarehe 15 Juni 2025. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TAA, Flightlink itaanzisha safari ya kila siku kutoka Arusha kwenda Nairobi, ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za usafiri wa anga katika ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania. Katika maandalizi ya safari hizo,TAA ikishirikiana na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, iko mbioni kukamilisha mfumo wa upokeaji na upangaji wa maafisa wa uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Arusha ili kuhakikisha safari hizo zinafanyika kwa ufanisi. TAA imesisitiza kuwa inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa anga kuhakikisha huduma bora kwa abiria na kuwezesha maoni kutoka kwa watumiaji wa viwanja vyake ili kuboresha huduma zaidi. #Airlines #flightlink #aviationlovers #aviationcareer #ys #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKZPgzoMsxD/?igsh=YTdveW5ndnF5ZnRt *TAA yatangaza kuanza Kwa safari mpy...

Aviation Tanzania on Instagram: "Utalipia $14,000 kwa Saa moja kuwa ndani ya ndege ya kifahari iliyopambwa kama hoteli ya nyota Tano. Jiji la Dubai linaendelea kuwa kitovu cha starehe na maisha ya kifahari na hivi sasa ndani ya jiji hilo,kuna huduma ya kipekee ya ndege binafsi inayokodishwa kwaajili ya sherehe zinazofanyika angani. Ni ndege binafsi inayomilikiwa na Kabir Mulchandani,mmiliki wa hoteli za FIVE Hotels and Resorts, iliyopambwa katika mandhari ya kifahari kama hoteli, na hukodishwa kwa sherehe au safari binafsi za anga. Ndege hii ina uwezo wa kubeba watu 16 na imepambwa na vifaa vya kisasa kama taa za LED, mfumo wa sauti wa kiwango cha kumbi za starehe, runinga kubwa, kitanda cha kifalme na bafu la ndani, mandhari Sawa na ilivyo katika hoteli za kifahari. Kwa gharama ya dola 14,000 kwa saa moja, mtu yeyote anaweza kukodisha ndege hii kwa ajili ya sherehe au safari za kifahari, hata kama hatumii huduma ya hoteli. Ndege hii, inayoitwa 9H-FIVE, ni mfano wa Airbus ACJ 220 na inafanya safari zake kwenda maeneo kama Santorini, Ibiza, au Zurich. Mwanzilishi wa FIVE Hotels, anasema huduma hii ni njia ya kuwapatia wateja huduma ya kipekee na yenye kukumbukwa. #5starhotels #fivehoteldubai #passengerexperience #airbusacj220 #9hfive #aviationlovers #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviata"

https://www.instagram.com/p/DKW8t3sMeZe/?igsh=MTFydThrbGc1ZXZpbw== *Utalipia $14,000 kwa Saa moja k...

Aviation Tanzania on Instagram: "Air Tanzania yafanya safari maalum kuwasafirisha mahujaji 105 kuelekea Hijja Shirika la Ndege la Air Tanzania @airtanzania_atcl limefanya safari maalum, kuwasafirisha mahujaji 105 kuelekea mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia, kwa ajili ya ibada ya Hijja ya mwaka huu. Kupitia taarifa rasmi, Air Tanzania imetoa shukrani za dhati kwa heshima waliyopewa na Baraza Kuu la Kiislamu kwa kulichagua shirika hilo kusafirisha mahujaji katika safari hiyo takatifu. Mwezi Machi mwaka huu, Shirika la Air Tanzania lilianza maandalizi ya kutumia ndege yake aina ya Boeing 737-9 kwa ajili ya kuwasafirisha waumini wa Kiislamu kwenda Saudi Arabia kwaajili ya ibada ya Hijja. Taarifa ya maandalizi hayo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, machi 31 2025, alipohutubia Baraza la Eid lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kwa wakati huo, Air Tanzania ilikuwa kwenye hatua ya kuomba vibali kutoka katika mamlaka husika ili kuanza rasmi safari hizo. #airlines #airtanzania_atcl #flywithairtanzania #hijja #aviationlovers #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviata"

https://www.instagram.com/p/DKSExbgMLMw/?igsh=MWlya2xmczg5cGVzYQ== *Air Tanzania yafanya safari maa...

Aviation Tanzania on Instagram: "Precision Air’s ATR 42-500, with registration number 5H-PWE, departing from Julius Nyerere International Airport. #airline #precisionair #pw #youarewhywefly #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKHC8mXswO4/?igsh=MTUyeWthaDNvZzNmZQ== *Precision Air ATR 42-500 Dep...

Aviation Tanzania on Instagram: "Malaysia Airlines yazindua Airbus A330 yenye chapa ya timu ya Manchester United. @malaysiaairlines imezindua ndege aina ya Airbus A330 iliyopakwa rangi na chapa ya klabu ya Manchester United, ikiwa tayari imefanyiwa majaribio ya kuruka angani. Ndege hiyo itatumiwa kuwasafirisha wachezaji wa Manchester United kutoka Kuala Lumpur kwenda Hong Kong kwa ajili ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya timu ya wawakilishi wa Hong Kong, China, katika Uwanja wa Hong Kong Ijumaa ya tarehe 30 Mei 2025. Mechi hii ni sehemu ya ziara baada ya msimu ya Manchester United barani Asia, ambapo kabla ya kufika Hong Kong, watacheza dhidi ya ASEAN All Stars huko Kuala Lumpur, Malaysia, tarehe 28 Mei 2025. Kwa kusherehekea uzinduzi huu, mashabiki wanapata punguzo la hadi 50% kwa safari za kwenda Kuala Lumpur na Hong Kong. #airline #malaysiaairlines #manchesterunited #manufans #a330 #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKEKjixs9VT/?igsh=MWJ3N3J5dnlhMXBjZw== *Malaysia Airlines yazindua Airb...

Aviation Tanzania on Instagram: "Air Tanzania yajipanga kuanza safari za ndani na nje ya nchi Katika maeneo haya. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la @airtanzania_atcl , Mhandisi Peter Ulanga, ametaja maeneo kadhaa ndani na nje ya nchi yanayohitaji kwa kiwango kikubwa huduma ya usafiri wa anga, akieleza kuwa tayari imeanza kuweka mipango kwa ajili ya kufanikisha huduma hizo. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la TBC, Mhandisi Ulanga alisema kuwa ndani ya nchi, maeneo ya Musoma, Shinyanga na hasa Bukoba yanaonesha uhitaji mkubwa wa huduma za ndege na kubainisha kuwa Bukoba ndiyo eneo lenye mahitaji ya juu zaidi, huku serikali ikiwa tayari imewekeza katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo hayo. Kwa upande wa safari za kimataifa, Mhandisi Ulanga alieleza kuwa taifa jirani la Msumbiji limeomba Air Tanzania kuanzisha safari zake kuelekea miji ya Maputo, Beira, Nampula na Pemba. Aidha, shirika hilo pia linaangazia uwezekano wa kuanzisha safari kuelekea visiwa vya Mayotte na Shelisheli, maeneo maarufu kwa vivutio vya utalii na biashara. Katika mipango yake ya ndani zaidi, Air Tanzania inatarajia kufungua safari za moja kwa moja kuelekea visiwa vya Pemba, Mafia na hifadhi ya Serengeti, hasa wakati wa msimu wa utalii, hatua ambayo inalenga kuimarisha utalii wa ndani na kuongeza mapato kwa taifa. Hadi sasa, Shirika la Ndege la ATCL linahudumia maeneo 14 ndani ya nchi. Katika bara la Afrika, linatoa huduma katika vituo 10, na nje ya Afrika linafika katika vituo vitatu. #routeexpansion #airline #airtanzania #airtanzania_atcl #aviationcareer #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DJ_P3Qas5B2/?igsh=ZDNzY2o3cnBqb3Z4 *Air Tanzania yajipanga kuanza sa...

Aviation Tanzania on Instagram: "Kuelekea uzinduzi wa Safari za Arusha–Nairobi, Flightlink yatambuliwa rasmi na na KATA. Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Kampuni ya ndege ya @flightlinktz kuzindua rasmi safari kati ya miji ya Arusha-Nairobi,kampuni hiyo imepokea rasmi Cheti na Uanachama kutoka Chama cha Wakala wa Usafiri wa Ndege Kenya (KATA). Hii ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo katika kuhakiki huduma bora na za kuaminika kwa wateja wake. Kupitia uanachama huu, Flightlink sasa inatambuliwa rasmi kama mshirika wa KATA chama cha kitaaluma kinachowakilisha na kusimamia maslahi ya mawakala wa usafiri nchini Kenya. Flightlink inatarajia kuzindua safari za anga kati ya mji wa Arusha na Nairobi kuanzia mwezi juni 15,2025 ,Safari ambazo zinalenga kurahisisha usafiri kwa wasafiri wa kibiashara, watalii, na wale wanaosafiri kwa shughuli binafsi. #airline #flightlink #kata #routeexpansion #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DJ9D3MhsIiH/?igsh=aDhudnA2eGw3M2Zu *Kuelekea uzinduzi wa Safari za Arus...

Aviation Tanzania on Instagram: "Air Tanzania Yapunguza Ucheleweshaji wa Safari kutoka 80% hadi 10%. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Air Tanzania, Mhandisi Peter Ulanga, amesema shirika hilo limepunguza ucheleweshaji wa safari kutoka asilimia 80 hadi asilimia 10. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la TBC, Mhandisi Ulanga amesema kupunguza ucheleweshaji wa safari ni miongoni mwa vipaumbele alivyoviweka tangu alipoingia katika nafasi ya uongozi, kwa lengo la kurejesha imani kwa abiria. Aidha, amesema kipaumbele kingine ni jitihada za kufufua ndege ambazo zilikuwa katika matengenezo kwa muda mrefu. #flightdelays #airline #airtanzania #airtanzania_atcl #aviationcareer #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DJ8uejysz9H/?igsh=MTBvbTBiM3pwdW1meQ== *Air Tanzania Yapunguza Uchelewe...

Aviation Tanzania on Instagram: "Etihad is hiring for; Duty Supervisor(6) – Tunis, Manchester, Hong Kong, Hanoi, Chiang Mai, Johannesburg Sales Representative (2) – Hyderabad, Cochin Sales Operations Administrator (3) – Jakarta, Mumbai, Taipei A320 First Officer Assessment Event (4) – Rome, London (Gatwick), Milan, Madrid First Officer (5) – A320, 777/787 (Type & Non-Type Rated), 777 Cargo, A350/A380 Captain (2) – A320, A350/A380 Airport Manager (2) – Hanoi, Sochi Manager (4) – Talent Programs, Network Operations, Sales Global Accounts (USA), Business Performance (Data Products) Engineer (2) – MCC Duty Engineer (Structures), Data Engineer Analyst (2) – Digital Analyst, Senior Analytics Specialist Digital/Tech Roles (4) – Digital Analytics Manager, Azure Platform Administrator, Senior Solutions Architect (Cloud Native/CRM), Brand and Product Photographer Officer (4) – Ethics & Compliance, Finance BP (UAE National), Category (UAE National), Pricing Controller Cadet Technician (UAE National), Airport Operations (UAE National) Cabin Crew– Worldwide Cabin Maintenance Supervisor– (UAE National) Aircraft Technician – IFE– Abu Dhabi Ground Operations Duty Manager– Abu Dhabi Guest Services Agent – Abu Dhabi Material Handling Coordinator– (UAE National) Demand Manager– Abu Dhabi Pricing Manager– Abu Dhabi. Apply now via Etihad’s official careers website. #airline #etihadairways #aviationjobs #aviationcareer #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DJ8bayhs3Wk/?igsh=Yjd1OW12MzRybmxw *Etihad is hiring for;* Duty Supervi...