
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 16, 2025 at 09:45 AM
https://www.instagram.com/p/DK9QCgltxDb/?igsh=NjlkaTJnc3dzN3dk
*RC Makonda Ashuhudia Safari Mpya ya Flightlink Kutoka Nairobi Hadi Arusha.*
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, @baba_keagan , leo Juni 17,2025 ametembelea katika Uwanja wa Ndege wa Arusha na kushuhudia kwa mara ya kwanza safari mpya ya ndege ya shirika la Flightlink iliyoanzia Uwanja wa Ndege wa Wilson, jijini Nairobi, Kenya hadi uwanja wa ndege wa Arusha.
RC Makonda alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Uendeshaji wa Flightlink Bw.Jameel Kassam kuhusu umuhimu wa safari hizo kwa mkoa wa Arusha na maendeleo ya sekta ya utalii na biashara.
Safari hii mpya ya moja kwa moja kati ya Arusha (ARK) na Nairobi (WIL) ni ya kwanza kuanzishwa nchini Tanzania, safari ambayo hutumia muda wa Dakika 45.
#airlines #flightlink #newroute #routeexpansion #atr72 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates