Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #flightlink
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Mmoja wa abiria waliosafiri Kwa Mara ya kwanza kutoka Nairobi hadi Arusha (WIL–ARK),Kwa kutumia ndege za shirika la @flightlinktz ameielezea safari hiyo kuwa ya haraka na yenye urahisi mkubwa. #Airlines #flightlink #newroute #routeexpansion #airlinepassenger #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DK_33PYtyzw/?igsh=cGpwY3lrY2lmdGU3 Mmoja wa abiria waliosafiri Kwa M...
Aviation Tanzania on Instagram: "RC Makonda Ashuhudia Safari Mpya ya Flightlink Kutoka Nairobi Hadi Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, @baba_keagan , leo Juni 17,2025 ametembelea katika Uwanja wa Ndege wa Arusha na kushuhudia kwa mara ya kwanza safari mpya ya ndege ya shirika la Flightlink iliyoanzia Uwanja wa Ndege wa Wilson, jijini Nairobi, Kenya hadi uwanja wa ndege wa Arusha. RC Makonda alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Uendeshaji wa Flightlink Bw.Jameel Kassam kuhusu umuhimu wa safari hizo kwa mkoa wa Arusha na maendeleo ya sekta ya utalii na biashara. Safari hii mpya ya moja kwa moja kati ya Arusha (ARK) na Nairobi (WIL) ni ya kwanza kuanzishwa nchini Tanzania, safari ambayo hutumia muda wa Dakika 45. #Airlines #flightlink #newroute #routeexpansion #atr72 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DK9QCgltxDb/?igsh=NjlkaTJnc3dzN3dk *RC Makonda Ashuhudia Safari Mpya ya...
https://www.instagram.com/p/DK7j_6TNByQ/?igsh=MTlq...
https://www.instagram.com/p/DK7j_6TNByQ/?igsh=MTlqM21mcGV4M2M4ag== *Flightlink yazindua safari mpya...
Aviation Tanzania on Instagram: "Mkuu wa uendeshaji wa shughuli za shirika la ndege la Flightlink, @jfk_1 ameeleza Lengo la ushiriki wa kampuni ya @flightlinktz katika mkutano wa kimaendeleo katika sekta ya Anga wa Aviadev na faida ambazo shirika hilo limezipata tangu liliposhiriki katika mkutano huo Kwa Mara ya kwanza mwaka 2024 nchini Namibia. #Airlines #flightlink #aviadev #aviationcareer #aviadevafrica #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DK19N-Ttxz7/?igsh=OGp0cHhzM2lvZGhz Mkuu wa uendeshaji wa shughuli za...
Aviation Tanzania on Instagram: "Katika maonyesho ya @kilifair 2025, Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la @flightlinktz , @munawerdhirani ameeleza namna shirika hilo lilivyojipanga kuongeza safari za ndani na nje ya nchi. Safari hizo ni pamoja na zile kati ya Uwanja wa Ndege wa Arusha na uwanja wa ndege wa Wilson zitakazozinduliwa tarehe 15 Juni 2025, pamoja na safari kati ya Zanzibar na Jomo Kenyatta zitakazoanza tarehe 1 Julai 2025. Aidha, Flightlink imepanga kuanzisha safari kati ya Mwanza na Kilimanjaro, zitakazozinduliwa ndani ya mwezi Julai. #Airlines #routeexpansion #flightlink #aviationlovers #aviationcareer #atr72500 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DKoSH0Pt-2f/?igsh=MTd5YnNsd204dnNyZw== *Flightlink yapanga kuanzisha...
Aviation Tanzania on Instagram: "Flightlink yashiriki katika maonyesho ya Karibu Kilifair Arusha. Shirika la ndege la @flightlinktz , limeshiriki katika maonyesho ya kibiashara na Utalii ya Karibu Kilifair Kwa mwaka 2025. Maonyesho hayo yaliyozinduliwa siku ya Jana Juni 6,2025 yalihudhuriwa na mgeni rasmi, Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh.Dotto Biteko, yanafanyika katika viwanja vya Magereza jijini Arusha na yanatarajia kuhitimishwa siku ya kesho Juni 08,2025. Zaidi ya makampuni 500 kutoka Afrika mashariki yamepata fursa ya kuonyesha bidhaa na huduma zao katika maonyesho hayo Kwa mwaka huu, maonyesho ambayo yanatazamiwa kukuza zaidi sekta ya utalii wa ndani na nje ya nchi. Flightlink imepata fursa ya kuonyesha na kutangaza zaidi huduma ya safari zake ikiwemo safari mpya zinazotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni zikiwemo safari za ndani na nje ya nchi. Endelea kutufuatilia Kwa habari mbalimbali kuhusu maonyesho ya Karibu Kilifair 2025. #exhibition #airline #flightlink #newroutes #routeexpansion #ys #kilifair2025 #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"
https://www.instagram.com/p/DKm9B4wNwpQ/?igsh=MWhubHIxdXJnM2M3NQ== *Flightlink yashiriki katika mao...
Aviation Tanzania on Instagram: "TAA yatangaza kuanza Kwa safari mpya za shirika la ndege la Flightlink. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania @tanzaniairports imetangaza kuanza kwa safari mpya za anga za shirika la ndege la @flightlinktz kati ya miji ya Arusha na Nairobi, kuanzia tarehe 15 Juni 2025. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TAA, Flightlink itaanzisha safari ya kila siku kutoka Arusha kwenda Nairobi, ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za usafiri wa anga katika ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania. Katika maandalizi ya safari hizo,TAA ikishirikiana na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, iko mbioni kukamilisha mfumo wa upokeaji na upangaji wa maafisa wa uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Arusha ili kuhakikisha safari hizo zinafanyika kwa ufanisi. TAA imesisitiza kuwa inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa anga kuhakikisha huduma bora kwa abiria na kuwezesha maoni kutoka kwa watumiaji wa viwanja vyake ili kuboresha huduma zaidi. #Airlines #flightlink #aviationlovers #aviationcareer #ys #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DKZPgzoMsxD/?igsh=YTdveW5ndnF5ZnRt *TAA yatangaza kuanza Kwa safari mpy...
Aviation Tanzania on Instagram: "Kuelekea uzinduzi wa Safari za Arusha–Nairobi, Flightlink yatambuliwa rasmi na na KATA. Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Kampuni ya ndege ya @flightlinktz kuzindua rasmi safari kati ya miji ya Arusha-Nairobi,kampuni hiyo imepokea rasmi Cheti na Uanachama kutoka Chama cha Wakala wa Usafiri wa Ndege Kenya (KATA). Hii ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo katika kuhakiki huduma bora na za kuaminika kwa wateja wake. Kupitia uanachama huu, Flightlink sasa inatambuliwa rasmi kama mshirika wa KATA chama cha kitaaluma kinachowakilisha na kusimamia maslahi ya mawakala wa usafiri nchini Kenya. Flightlink inatarajia kuzindua safari za anga kati ya mji wa Arusha na Nairobi kuanzia mwezi juni 15,2025 ,Safari ambazo zinalenga kurahisisha usafiri kwa wasafiri wa kibiashara, watalii, na wale wanaosafiri kwa shughuli binafsi. #airline #flightlink #kata #routeexpansion #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DJ9D3MhsIiH/?igsh=aDhudnA2eGw3M2Zu *Kuelekea uzinduzi wa Safari za Arus...